Header Ads Widget

MBUNGE BUTONDO ATOA VIFAA VYA MICHEZO VYA MILIONI 1.8

Katibu wa Mbunge Godfrey Mbussa akigawa vifaa vya michezo kwa niaba ya Mbunge Butondo.

MBUNGE BUTONDO ATOA VIFAA VYA MICHEZO VYA MILIONI 1.8

MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo ametoa vifaa vya michezo kwa timu za mipira wa miguu Kata ya Masanga wilayani Kishapu.

Ugawaji wa vifaa hivyo vya michezo umefanyika leo Agosti 17,2024 katika bonanza la michezo lililoandaliwa na diwani wa  Masanga Enock Reuben.

Butondo amewakilishwa na Katibu wake Godfrey Mbussa, ambaye amesema utoaji wa vifaa hivyo vya michezo, una jumuishi mipira saba, na jezi zake,na kwamba kila kijiji kimepata vifaa hivyo "pair"moja moja.

"Vifaa vya michezo ambavyo ametoa mbunge vina thamani ya Sh.milioni 1.8," amesema Godfrey.

Aidha, 
katika Bonanza hilo diwani wa Masanga Enock Reuben ametoa zawadi ya Sh.elfu 40 kwa washindi wa kwanza na wapili, huku akimshukuru Mbunge Butondo kwa kumuunga mkono ili kukuza michezo.

Post a Comment

0 Comments