Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI 10 YA MAENDELEO WILAYANI KISHAPU

MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI 10 YA MAENDELEO WILAYANI KISHAPU

Na Marco Maduhu,KISHAPU
MWENGE wa uhuru ukiwa wilayani Kishapu umekagua,kuzindua,kuona na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi 10 ya maendeleo.

Mwenge wa uhuru umewasili leo Agosti 10,2024 mkoani Shinyanga, ambao utakimbizwa katika halmashauri sita za mkoa huo, ambapo umeanzia wilayani Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema Mwenge ukiwa wilayani Kishapu utakimbizwa kilomita 91.5 na kupitia miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya Sh.bilioni 3.5.

"Miradi hii 10 ya maendeleo ambayo itapitiwa na mwenge wa uhuru imo ya elimu,afya,uchumi,miundombinu ya barabara pamoja na maji,"amesema Mkude.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava, akizungumza kwenye miradi hiyo, amesema miradi yote ambayo imepitiwa na mwenge huo inapaswa kutunzwa na kuendelezwa ili ipate kutoa huduma stahiki kwa wananchi na wanafunzi.

Aidha,akitoa salama za Mwenge ametoa wito kwa wananchi kwamba wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na kuchagua wagombea wenye sifa na siyo watoa rushwa ambao hawawezi kuwaletea maendeleo.
Pia, amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti, na kuacha kukata miti hovyo pamoja na kutunza vyanzo vya maji.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru 2024 inasema"Tunza mazingira na Shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu"
Mwenge huo wa uhuru kesho utakimbizwa katika Manispaa ya Shinyanga.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇

Post a Comment

0 Comments