Header Ads Widget

BUTONDO AWAUNGA MKONO WANASIMBA KIJIJI CHA MWAMASHIMBA KUSHEREHEKEA SIMBA DAY,AMWAGA MINOTI

BUTONDO AWAUNGA MKONO WANASIMBA KIJIJI CHA MWAMASHIMBA KUSHEREHEKEA SIMBA DAY, AMWAGA MINOTI

Na Marco Maduhu

Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniphace Butondo, amewaunga mkono mashabiki wa timu ya Simba katika kijiji cha Mwamashimba kata ya Mwamalasa, wilaya ya Kishapu, kusherehekea Simba Day.

Katika sherehe hiyo, Mbunge Butondo, ambaye ni shabiki wa timu ya Yanga, ameeleza kuwa ameshiriki na wananchi hao kwa ajili ya kuunga mkono sherehe hiyo ya Simba Day, na kutoa mchango wa Shilingi laki 2 kwa ajili ya kuongeza furaha yao.

Simba Day,ambayo huadhimishwa kila mwaka, hutumika pia kutambulisha wachezaji wapya wa timu hiyo.

Tamasha la mwaka huu la Simba day nila 16, ambapo wachezaji wa msimu wa 2024/2025 wametambulishwa.

Post a Comment

0 Comments