MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI 8 YA MAENDELEO MANISPAA YA KAHAMA YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 13.9


MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI 8 YA MAENDELEO MANISPAA YA KAHAMA YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 13.9

Na Marco Maduhu,KAHAMA
MWENGE wa uhuru umekimbizwa Manispaa ya Kahama umbali wa kilomita 64.8 na kumulika jumla ya miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya Sh.bilioni 13.9.

Mwenge huo umekimbizwa leo Agosti 15,2024 ukitokea halmashauri ya Ushetu.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava, akizunguza kwenye miradi hiyo ya maendeleo, ambayo baadhi aliizindua, kuifunga, kuona na kuweka jiwe la msingi, ameipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa kutenda mapato yake ya ndani na kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Nimefurahishwa sana na Manispaa ya Kahama, mmekuwa mkitenga mapato yenu ya ndani na kurudisha kwa wananchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo,”amesema Mnzava.
Aidha, amewataka pia wananchi wa Kahama waitunze pia miundombinu ya miradi ya maendeleo ambayo imepitiwa na mwenge huo wa uhuru ili ipate kuwa hudumia kwa muda mrefu.

Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masudi Kibetu akipokea mwenge huo wa uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushetu Hadija Kabojela, amesema utakimbizwa kilomita 64.8 na kumulika miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya Sh.bilioni 13.9.
Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu 2024, inasema"Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu".

Mwenge huo kesho utakabidhiwa mkoani Tabora.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masudi Kibetu (kulia)akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushetu Hadija Kabojela.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiwa ameshika mwenge wa uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masudi Kabetu akiwa wameshika mwenge wa uhuru.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464