Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI SESEKO-NGUNDANGALI WILAYANI KISHAPU

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI SESEKO-NGUNDANGALI WILAYANI KISHAPU

Na Marco Maduhu,KISHAPU
MWENGE wa uhuru umezindua mradi wa maji wa ziwa victoria wa Seseko,Ngundangali wilayani kishapu ambao utahudumia wananchi wapatao elfu 15,500.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava, amezindua rasmi mradi huo leo Agosti 10,2024 huku akiipongeza Ruwasa kwa utekelezaji wa mradi huo ambao umemtua ndoo kichwani mwanamke.
Akizungumza kwenye mradi huo amewataka wananchi waendelee kuitunza miundombinu ya maji na vyanzo vya maji ili iendelee kuwa hudumia kwa muda mrefu na kutatua changamoto za ukosefu wa maji.

"Wananchi itunzeni miradi hii pamoja na vyanzo vya maji ili iwe endelevu,"amesema Mnzava.
Pia,amewapongeza Ruwasa kwa kutangaza zabuni ya utekelezaji wa mradi huo kupitia mfumo wa kidigital.

Naye Meneja wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilayani Kishapu Mhandisi Dicksoni Kamazima, awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, amesema utahudumia vijiji vya Seseko,Mpumbula, Kakola,Dugushi na Ngundangali, na kutoa huduma kwa wananchi elfu 15,500 na gharama zake ni Sh.bilioni 2.8.
Amesema kwamba mradi huo una vituo vya kuchotea maji 31 ambavyo vitamundolea adha mwananchi hasa wanawake kufuata maji umbali mrefu.

Mwenge huo wa uhuru ukiwa wilayani Kishapu umekimbizwa kilomitab 91.5 umezindua,kuona na kuweka jiwe la msingi miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya Sh.bilioni 3.5.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru kitaifa 2024 inasema"Tunza mazingira na Shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu".

Post a Comment

0 Comments