INEC IMETOA WITO KWA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUBORESHA TAARIFA ZAO DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA,YATAHADHARISHA WASIJIANDIKISHE MARA MBILI WATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA
TUME huru ya Taifa ya uchaguzi Tanzania (INEC)imetoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye vituo ili kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, huku ikitoa tahadhari kwao wasijiandikishe mara mbili watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kulipa faini au kufungwa jela.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 9,2024 na Makamu Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC)Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mbarouk Mbarouk kwenye mkutano wa tume hiyo na wadau wa uchaguzi mkoani Shinyanga.
Amesema wadau hao wa uchaguzi wakawe mabalozi wazuri kwa wananchi kwa kuwapatia taarifa sahihi na kuwahamasisha wajitokeze kwa wingi kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga, pamoja na kuwaambia wasijiandikishe mara mbili kwenye daftari hilo, kwamba watakao kamatwa watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
“Kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ni kosa kisheria na adhabu yake ni faini ya Shilingi 100,000 hadi 300,000, na kifungo ni miezi 6 hadi miaka 2 au vyote kwa pamoja,”amesema Jaji Mstaafu Mbarouk.
“Katika vituo vya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura, kila chama cha siasa kinapaswa kuweka wakala mmoja ili kujiridhisha kwamba watu wanao wanaofika kujiandikisha kama wana sifa,”ameongeza Mbarouk.
Aidha, amesema zoezi hilo la uboreshaji taarifa kwenye daftari la mpiga kura katika mkoa wa Shinyanga na Mwanza litaanza Agosti 21 hadi 27, 2024 na kwamba uzinduzi wa uboreshaji wa daftari huo ulishafanyika mkoani Kigoma Julai 20 mwaka huu na Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Katika hatua nyingine amesema katika zoezi hilo la uboreshaji taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kuwa watu wenye ulemavu, wazee pamoja na wanawake wenye watoto wachanga watapewa kipaumbe na hakuna kupanga foleni.
Naye Mkurugenzi wa huduma za sheria tume huru ya taifa ya uchaguzi Mtibora Seleman, akiwasilisha mada ya taarifa ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura, amesema maadalizi yote yamekamilika na kwamba vituo 40,216 vitatumika kuandikisha wapiga kura, na vituo 39,709 vipo Tanzania, na 417 Zanzibar, na kwa Mkoa wa Shinyanga vipo 1,339.
Amesema pia kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kwamba wanatarajia kuandikisha wapiga kura wapya milioni 5.5 sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura 29,754,699 waliopo kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/2020.
Amesema kwamba pia wapiga kura milioni 4.3 wanatarajiwa kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
“Katika Mkoa wa Shinyanga tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 209,951 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 ya wapiga kura 995,918 waliopo kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, na tunatarajia baada ya uandikishaji huu Mkoa wa Shinyanga utakuwa na wapiga kura 1,205,869,”amesema Seleman.
Nao wadau wakichangia mada kwenye mkutano huo, walishauri zoezi hilo lifanyike kwa ufanisi pamoja na kuandikisha watu sahihi wenye sifa wakiwamo wafungwa kwenye magereza ili kusiwepo na mkanganyiko.
Aidha, wadau walioshiriki kwenye mkutano huo ni viongozi wa dini, kimila, vyama vya siasa, asasi za kiraia, watu wenye ulemavu, kamati ya ulinzi na usalama mkoa, na vyombo vya habari.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkutano wa tume huru ya taifa ya uchaguzi INEC na wadau wa uchaguzi mkoani Shinyanga ukiendelea.
Makamu Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC) Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mbarouk Mbarouk akizungumza kwenye mkunao huo.
Mjumbe wa tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC) Mheshimiwa Balozi Mapuri akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa wa tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC)Giveness Aswile akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa huduma za sheria tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC)Mtibora Seleman akiwasilisha mada ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi msaidizi idara ya daftari na TEHAMNA Mbanga Rubibi,akiwasilisha mada ya mfumo wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na vifaa vinavyotumika kwenye mkutano huo.
Menejimenti ya tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC) ikiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano wa wadau wa uchaguzi na tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC)kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ukiendelea mkoani Shinyanga.

Viongozi wakiwa meza kuu.
Picha za pamoja zikipigwa.
picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464