Suzy Butondo Shinyanga press blog
Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Maofisa kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa ambao ni Isack Maswi, Silyvester Lugata Selanyika Athumani kwa tuhuma za kujihusisha na kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo leseni za watoa huduma ndogo ndogo za fedha daraja la pili.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi leo ofisini kwake amesema watuhumiwa hao wamekamatwa jana, wawili wamekamatiwa Shinyanga na mmoja amekamatiwa mkoani Mara, hivyo wanatarajia kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.
Magomi amesema watoa huduma ndogo za fedha wamejikita kwenye changamoto ya kupata leseni bandia kutoka kwa watu wachache ambao ni matapeli, hivyo amewahimiza wananchi wote kutembelea Benki kuu na Matawi yake pale wanapokuwa wanahitaji leseni za watoa huduma ndogo za fedha daraja la pili.
"Endapo kuna mfanyabiashara yeyote wa Microfinance anahitaji juu ya upatikanaji wa leseni yake atembelee tawi lolote la karibu la Benki kuu,nayasema haya kwa sababu wapo watu wametapeliwa, benki kuu inatoa leseni kwa makampuni shilingi laki tano 500,000 na kwa mtu binafisi shilingi laki tatu 300,000, lakini matapeli hao wanaenda kutoa leseni mpaka milioni 3.wengine mpaka milioni 10.
Kamanda wa jeshi la polisi ametoa wito kwa watu wanaojishughulisha na microfinance wafuate taratibu,sheria na kanuni zilizopo, hivyo oporesheni hii ni endelevu na wale watakaobainika kwenda kinyume na kuchukua kadi za watu watachukuliwa hatua kali, "huku mitaani wanaita mikopo umiza"