Header Ads Widget

JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKAMATA WATUHUMIWA WA UTOROSHAJI WA MADINI SITA


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha milungi iliyokamatwa

Suzy Butondo Shinyanga press Blog

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limewakamata watuhumiwa wawili wakiwa na madini aina ya dhahabu vipande vitatu (03) vilivyochomwa, vyenye uzito wa gramu 13,35 na mzani mmoja (01) pamoja na pesa Tsh. 2,799,000.

Licha ya kukamata dhahabu hizo
Pia Agosti 1, 2024 katika Kata ya Nyasubi, Manispaa ya Kahama, walikamatwa watuhumiwa wanne wakiwa na madini yadhaniwayo kuwa ya dhahabu vipande 11 vyenye uzito wa gramu 652.6, gari aina ya SUZUKI VITARA, pamoja na pesa shilingi 96,000,000, na watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Shinyanga SACP Janeth Magomi leo julai 21,8,2024 amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka yao.

Magomi pia amesema Jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa mmoja pamoja na Gari aina ya TOYOTA HIACE yenye namba za usajili T. 886 DCU akiwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi bunda 02 zenye uzito wa gramu 400.

Aidha Magomi amesema walipata taarifa fiche kwamba Gari aina ya TOYOTA HIACE inayofanya safari zake Shinyanga - Kahama inasafirisha dawa za kulevya, wakaweka mitego, wamekuta Mirungi bunda 02 zenye uzito wa gramu 400, na mtuhumiwa wamemkamata.

"Tunatoa Onyo kwa wanaofanya biashara ya dawa za kulevya, wanaosafirisha dawa za kulevya waache mara moja, kwani taarifa tunazo, naomba wananchi tuendelee kupeana taarifa za uhalifu na wahalifu",amesema Magomi.

Magomi amevitaja vitu vingine vilivyokamatwa ni pikipiki 06, nondo vipande 12, simu 04, kaboni mifuko 02, Godoro 02, Redio 03, jiko la gesi 01, pipa 01 la kuchenjulia dhahabu na Ving'amuzi 02.

Pia amesema kesi 20 zimepata mafanikio mahakamani, ambapo kesi 01 ya mauaji kesi 04 kubaka washtakiwa 02 walihukumiwa kunyongwa hadi kufa, washtakiwa 04 walihukumiwa kifungo miaka 30 jela, kesi 01 ya kujiwasilisha (impersonation) mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo miaka 18 jela, kesi 03 kujeruhi washtakiwa 05 walihukumiwa kifungo miaka 05 jela, kesi 01 kuharibu mali washtakiwa 02 walihukumiwa kifungo miaka 03 jela, kesi 02 ajali kugonga watembea kwa miguu na kusababisha majeruhi washtakiwa 02 walihukumiwa kifungo miaka 02 jela.

"Tumepata mafanikio ya kesi 03 za wizi washtakiwa 03 walihukumiwa kifungo miezi mitano jela, kesi 01 kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo miezi minne jela, kesi 01 shambulio la kudhuru mwili mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo miezi 03 jela na kesi 03 kuingia kwa jinai washtakiwa 03 walihukumiwa kifungo miezi 03 jela",amesema.

Aidha amebainisha kuwa Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia kikosi cha Usalama barabarani wamefanikiwa kukamata jumla ya makosa 3,084 ambapo makosa ya magari ni 2,082 na makosa ya bajaji na pikipiki ni 1,002 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa hapo, pia Madereva 02 wamefungiwa leseni ya udereva kwa kipindi cha miezi mitatu kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya watu watatu.

Kuhusu utoaji wa elimu ,Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kufanya jumla ya mikutano 84 ya uelimishaji kwa jamii ambapo jumla ya vikundi 41 vya ulinzi shirikishi vimepewa mbinu za kudhibiti matukio ya uhalifu pamoja na elimu ya ukamataji salama.

"Tunaishukuru jamii kwa kuendelea kutoa ushirikiano madhubuti katika kuhakikisha Usalama wa mkoa wa Shinyanga una kuwa shwari sambamba na kupokea elimu inayotolewa, pia ninatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutii na kufuata taratibu na kanuni za nchi"amesema Magomi.

















Post a Comment

0 Comments