MASHABIKI SIMBA MKALAMA WATOA MSAADA HOSPITALI YA WILAYA NA SHULE YA SEKONDARI NDUGUTI

   

Mashabiki wa Simba Wilayani Mkalama leo Agosti 3,2024 wameadhimisha Simba Day kwa kutoa msaada katika hospitali ya Wilaya pamoja na shule ya sekondari Nduguti.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo, kiongozi wa mashabiki wa Simba wilayani Mkalama, Bwana Tesha Daniel amewaomba wananchi Mkalama kuwa na tabia ya kujitolea katika matukio ya kijamii kwa kutoa msaada mbalimbali kwa watu wenye uhutaji kwa lengo la kujenga jamii yenye upendo na amani.

"Tuifanye dunia kuwa sehemu salama, tunawajibu wa kujitolea pale inapobidi kwa ajilii ya kuleta tabasamu kwa ndugu zetu, niwaombe tuwe na desturi kama hii ya kuitika pale tunapoitwa kwa ajili ya wengine" Tesha 

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nduguti, Rosemary Richard ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Nne amewashukuru mashabiki wa Simba kwa upendo wao na kuwaomba wananchi wilayani Mkalama kuiga mfano wa mashabiki hao wa Simba. 


Vifaa vilivyotolewa na mashabiki wa Simba leo katika wodi ya wazazi ya hospitali ya Wilaya ni pamoja na Sabuni, Sukari na kwa upande wa shule ya sekondari Nduguti mashabiki hawa wametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wakike  pamoja na sabuni kwa wanafunzi wa kiume
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464