MBUNGE MPINA ATINGA JIMBONI KISESA! AWAFAFANULIA WANANCHI KUHUSU SAKATA LA SUKARI!

Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina akizungumza kwenye mkutano wake katika kata ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu

  • Suzy Butondo, Shinyangapress blog

    MBUNGE wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu, Luhaga Mpina ameendelea kusimama na msimamo wake alioutoa bungeni na kusababisha kusimamishwa kuhudhuria mikutano 15 ya bunge ambapo amesisitiza mbele ya wapiga kura wake wa Jimbo la Kisesa kwamba madai yake yalikuwa sahihi.

    Akihutubia maelfu ya wapiga kura wake wa Jimbo la Kisesa mjini Mwandoya wilayani Meatu, Agosti 11, 2024 Mpina amesema pamoja na hoja yake kutopatiwa majibu bungeni sasa ameamua kutafuta haki yake katika vyombo vya sheria, ambapo amefungua kesi tatu na kesi hiyo itaanza kusikilizwa rasmi katika Mahakama Kuu mnamo Agosti 28, 2024.

    Huku akishangiliwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika mjini Mwandoya wilayani Meatu mkoa wa Simiyu, Mpina amefafanua kuhusu misamaha ambayo ilitolewa kwa wafanyabiashara waliosamehewa kodi na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi.

    Amesema pamoja na Serikali kuwasamehe wafanyabiashara hao ambao hata hivyo baadhi yao hawajishughulishi na biashara ya uuzaji wa sukari na wao kuingiza sukari hiyo pasipo kuilipia kodi yoyote bado sukari iliendelea kuuzwa kwa wananchi kwa bei ya juu huku baadhi ya viwanda vya sukari hapa nchini vikipata hasara.

    “Tulitegemea baada ya Serikali kutoa misamaha hiyo ambayo mimi binafsi naiita ni “misamaha haramu” watanzania wanyonge katika nchi hii wangepata nafuu ya bei, na hapo msamaha ambao umetolewa ungekuwa na maana kwao, na ungewapunguzia makali ya bei ya sukari, sasa tunauliza palikuwa na sababu gani ya kutolewa kwa misamaha hiyo wakati wananchi waliendelea kuuziwa sukari kwa bei kubwa,”

    “Watanzania wengi hawakuelewa nilichokuwa nakihoji bungeni, sasa nimekuja kwenu kuwafafanulia ili muelewe kwa kina na msipotoshwe na madai ya baadhi ya wachache hapa nchini wanaodai eti Mpina anaishambulia Serikali, kilichopaswa kufanyika baada ya sukari kuingia nchini, wananchi wangenufaika kwa kuuziwa kwa bei ya chini kwa vile Serikali yao tayari iliisha toa msamaha kwa wafanyabiashara hao ambao waliingiza sukari hiyo pasipo kulipia kodi yoyote ile lakini haikuwa hivyo,” ameeleza Mpina.

    Kwa upande wake mmoja wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Meatu na ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Donald Magina amewataka wakazi wa Jimbo la Kisesa waendelee kumuunga mkono mbunge wao kutokana na kazi kubwa anayoifanya katika kuwaletea maendeleo na kutetea maslahi ya Taifa.

    Mkutano huo pia umehudhuriwa na marafiki wa Luhaga Mpina, maarufu kwa jina la Friends Of Mpina Group ambao wamepata fursa kutoa salaam zao kwa wakazi wa Jimbo la Kisesa na wakawaomba wasimtupe mkono mbunge wao bali waendelee kumuunga mkono ili aendelee kuwapigania katika kuwaletea maendeleo na kutetea maslahi ya Taifa kwa ujumla.

    Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Katibu wa CHADEMA kata ya Bukundi Meatu Simiyu Patrick Makwaya na Katibu wa hamasa wa Chama cha ACT Wazalendo kutoka kata hiyo ya Bukundi wameungana na wanachama wa CCM kumuunga mkono mbunge Mpina.

    Wanachama hao wamesema wametoa zawadi ya ng’ombe mmoja kwa mbunge Mpina ambaye atamuuza na fedha yake itasaidia kulilipa Jopo la Mawakili ambalo litamtetea Mpina kwenye kesi zake alizofungua ikiwemo ile ya Mheshimiwa Spika, Dkt. Tulia Ackson akipinga kutakiwa kutohudhuria mikutano 15 ya bunge.

    Kwa upande wao wananchi wa Jimbo la Kisesa kwa kauli moja wamesema wanamuunga mkono mbunge wao na kwamba hoja zake anazozitoa bungeni ni sahihi zenye mlengo wa kutetea maslahi ya Taifa na kwamba badala ya kuadhibiwa ilikuwa busara bunge ingezifanyia kazi na kupata ukweli wake na kama ni adhabu basi ingechukuliwa baada ya kubainika hoja za Mpina si za kweli, hapo hata wao wasingetia neno lolote la kumuunga mkono.

    Agnes Baya amesema mkutano ambao umefanyika umeonesha jinsi gani wananchi wake bado wanamuunga mkono na kwamba wako pamoja naye na wataendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu kwa vile ni mmoja wa viongozi wanaotetea maslahi ya Taifa na siyo maslahi yake binafsi.

    Wananchi hao pia wameendesha harambee ya papo kwa papo na kuweza kukusanya fedha ambazo wamemkabidhi mbunge Mpina ili zimsaidie katika malipo ya mawakili 100 ambao wamejitokeza kumtetea katika kesi zake akiwemo Rais mpya wa Chama cha Mawakili nchini (TLS), Boniface Mwambukusi.

    Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina akizungumza kwenye mkutano wake katika kata ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu

    Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina baada ya kumaliza kuongea kwenye mkutano wake akipokea fedha ambayo wanamchangia wananchi wa jimbo la Kisesa kwa ajili ya kuendesha kesi mahakamani kwenye mkutano wake katika kata ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu

    Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina akiwa kwenye mkutano wake kabla ya kuanza kuzungumza katika kata ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu
    Mmoja wa Marafiki wa mpina maarufu kwa jina la Friends Of Mpina Group   kutoka Mwanza wakizungumza kwenye mkutano huo ambapo waliahidi kushikamana nae mpaka kieleweke

    Stephano Nshimba Joseph mwanafunzi wa chuo kikuu sauti akizungumza kwa niaba ya marafiki wa mpina   maarufu kwa jina la Friends Of Mpina Group  kutoka chuo kikuu Sauti

    Wachungaji na Mashehe wakimuombea mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina ili aweze kushinda kesi ya kutetea rasilimali za wananchi ambao waliahidi kuendelea kumuombea
    Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kutoka kata ya Bukundi wilayani Meatu akizungumza kwenye kikao cha mbunge Luhaga Mpina
    Wananchi wakimchangia fedha Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina ili akaendelee na mahakama

    Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina akizungumza kwenye mkutano wake katika kata ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu
    Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina akiwa na viongozi mbalimbali kwenye mkutano wake katika kata ya Mwandoya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu
    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina
    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina
    Wananchi wa kata ya Mwandoya wilayani Meatu wakimshangilia mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina
    Wananchi wa kata ya Mwandoya wilayani Meatu wakimpokea mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wilayani Meatu wakimpokea kwa furaha na ndelemo mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina

    Mnunge wa jim la Kisesa Luhaga Mpina akpokelewa kwa bashasha na wananchi
    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wilayani Meatu wakimpokea kwa furaha na ndelemo mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina

    Wananchi wa kata ya Mwandoya wilayani Meatu wakimpokea kwa furaha na ndelemo mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464