Mheshimiwa Diwani wa kata ya Talaga Richard Dominick akizungumza baada ya michezo ya Rich Cup
Na Suzy Butondo, Shinyanyanga Press blog
Michuano ya Soka ya ligi ya Richi Cup imemalizika rasmi na Sinza Stars ya Ngunga wilayani kishapu mkoani Shinyanga kuibuka wababe wa ligi hiyo Baada ya kuiliza Chamazi Fm ya Nhobola kwa mikwaju 8 baada ya dakika 90 kumalizia bila kufungana.
Mashindano ya Richi Cup yamefanyika kata ya Talaga Kijiji cha Nhobola juzi 23/08/2024, ambapo kauli mbiu Ilikuwa ni vijana kuwakusanya pamoja kwa kufanya mazoezi ya utayari,kwa miili yao, kutokomeza ukatili wa kijinsia,urawiti,ushoga pamoja na kutokomeza mimba za Utotoni ikiwemo kuwalinda wanafunzi wa kike wanaosoma shule ya sekondari Talaga.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika Kocha wa timu ya Sinza stars Emmanuel Masanja amesema katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo walitolewa na kuingia katika hatua iliyofuata kwa nafasi ya Best Lozer jambo ambalo liliwafanya wajipange vyema na hatimaye kuwa mabingwa.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Talaga Richard Dominick ambaye ndiye mfadhili wa mashindano hayo amesema lengo la kuanzishwa kwa mashindano hayo ni kuwaweka Pamoja vijana ili washiriki katika mapambano ya ukatili wa kijinsia ubakaji na ulinzi katika jamii.
Diwani Dominick amesema Pamoja na malengo hayo ndoto iliyopo ni kuhakikisha wanaibua vipaji vya michezo kwa kuunda timu ya mpira wa miguu ya kata itakayoshiriki katika michezo ya kata na kata Jirani,na katika mashindano hayo yaliyoshirikisha Jumla ya timu 16 mshindi ameondoka na zawadi ya Sh 150,000. Pamoja na Jezi zenye thamani ya sh 200,000.
"Timu shiriki Zilikuwa 16, na
timu zilizoingia Fainal ni Sinza Star ya kijiji cha Ngunga na Chamazi ya kijiji cha Nhobola, ambapo timu ya Sinza Star Imeibuka kidedea kwa kumfunga Hasimu wake kwa Gori nane kwa saba kwa mikwaju ya Penart nakujinyakulia zawadi ya jezi pea moja, mpira wa miguu mmoja,firimbi moja,na sh 100,000."amesema Dominick.
Mshindi wa pili Chamazi Fc,alipata zawadi ya jezi pea Moja Mpira mmoja,filimbi Moja,na sh 50,000.huku
mshindi wa Tatu Geita Star ya Nhendegese ikijizolea zawadi jezi pea moja,mpira mmoja filimbi moja,na sh 30,000.Nafasi ya Nne imeshikwa na Jijongo A, ambayo imejinyakulia zawadi ya Jezi pea moja mpira mmoja filimbi Moja na Tsh 20,000.
Aidha Diwani wa Kata ya Talaga amemshukuru Mkurugenzi waJambo group Selemani Hamisi kwa kuwa mdau wa mashindano hayo ambapo alimpatia Mh diwani jezi, mipira, pamoja na Filimbi, lakini pia amemshukuru mkurugenzi wa kiwanda cha Gaki MNEC wa Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano mkubwa aliouonyesha kwa kumpatia vyombo vya Matangazo na anamuombea aendelee na moyo huo.
Pia alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo Nyangindu Ng"wanang"wanza kwa majitoleo yake ya kumpatia jezi,na mipira,kwa ajiri ya kufanikisha mashindano ya Rich Cup, ambapo pia anazishukuru timu zilizoshiriki,pamoja na wananchi wa kata nzima ya Talaga kwa kuendeleza kumpa Ushirikiano,
"Nawashukuru sana viongozi wangu wote mlionishika mkono kwa ajili ya kufanikisha mashindano haya, niwaombe muendelee kuwa na moyo huo wa ushirikiano na wa upendo, kwani kutoa ni moyo pia niwaombe vijana kupitia mashindano haya wabadilike wasijihusishe na mambo mbalimbali ya ukatili wa aina yeyote na kutokana na mmomonyoko wa maadili wajiepushe kujiingiza huko badala yake wakemee maovu ya aina yoyote ili kuhakikisha amani inatawala katika jamii yetu"amesema