Header Ads Widget

WAUMINI WATAKIWA KUSONGA MBELE NA IMANI YA YESU KRISTO, WASIKATE TAMAA NA KURUDI NYUMA WANAPOKUTANA NA MAJARIBU MBALIMBALI


Mwalimu wa theolojia kutoka chuo cha Calvary Mkoani Arusha Habakuki Siroko
akihubiri neno la Mungu katika kanisa la Philadelphia Miracle Temple Ndembezi

Suzy Butondo, Shinyanga press blog

Mwalimu wa theolojia kutoka chuo cha Calvary Mkoani Arusha Habakuki Siroko amewataka waumini wote waliookoka wasirudi nyuma wakaachana na imani ya Yesu kristo pale wanapokutana na changamoto za majaribu mbalimbali, badala yake wamwamini Mungu kwamba anaweza mambo yote hakuna kinachoshindikana.

Hayo ameyasema jumapili wakati akihubiri neno la Mungu katika ibada, iliyofanyika katika kanisa la Philadelphia Miracle Temple lililopo Ndembezi manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema kuna baadhi ya waumini wamekuwa wakipatwa na changamoto mbalimbali katika maisha yao wanarudi nyuma na kuacha wokovu, ambao wameokolewa kwa thamani kubwa.

Amesema ili wasirudi nyuma pale wanapopatwa na changamoto wanatakiwa kumtazama Yesu ambaye yeye alishinda changamoto za majaribu mbalimbali, hivyo wakimwendea yeye hakuna kinachoshindikana yote yanawezekana.

"Niwaombe ndugu zangu katika nyakati hizi tunapopatwa na majaribu ya aina yoyote tujikite kwenye maombi na tujifunze habari za Yesu, neno la Mungu likae kwa wingi ndani ya mioyo yetu, kama kuna jambo linakuchanganya sema pale msalabani yalikwisha, hivyo hata jaribu lako litakwisha kwa uweza wa Mungu kinachotakiwa ni kuwa na imani"amesema mwalimu Habakuki.

Pia amewataka waumini wote wawe watu wakuhudhulia ibadani, kwani ukiwa mtu wa kupenda ibadani itakuwezesha kukua kiroho, hivyo ni vizuri ukimwamini Mungu uweke mbele ratiba za ibada, kwani kuhudhulia kwenye ibada ni moja ya sadaka, hivyo Mungu awasaidie waweze kuhudhulia kwenye ibada kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu.

" Kama huna sababu za msingi huwezi kuacha kufika kwenye ibada maana ibada ni mahari ambapo Mungu anatuongeza kiwango cha imani ya kweli ambayo haifanani na imani za waganga wa kienyeji, mahali popote panapofanyika mambo makubwa kuna sadaka kwa sababu hata Yesu mwenyewe alitolewa sadaka"amesema Habakuki.

"Mfano Kornelio alikuwa Akida alikuwa mkuu wa majeshi ambaye sadaka yake ilipata kibali mbele za Mungu, hivyo na sisi Mungu anatuwazia mambo mazuri ambayo tukimwamini na tukajitoa kikamilifu tutauona ufalme wa mbinguni"amesema

Habakuki akizungumzia imani amesema imani huja kwa kusikia na imani lazima ipaliliwe kwa sababu inatengeneza njia mpya ya kufika mbinguni, kwani Yesu ni kila kitu ukimpata umepata kila kitu, hivyo amewashauri waumini wawe na imani ili wanapoomba waamini kuwa Mungu ametenda"ameongeza.

Amesema Yesu anawapenda wale wampendao na wale wamtafutao kwa bidii watamuona, hivyo amewaomba waumini wasikate tamaa pale wanapokutana na misukosuko ya kila aina wamtegemee Mungu, wahudhulie ibada kwa bidii kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu na waendelee kuhubiri neno la Mungu kwa watu ambao hawaijui kweli ili waweze kuijua kweli na waweze kuuona ufalme wa mbinguni.

"Cha muhimu zaidi tunapokuwa katika imani ya Yesu kristo tumwamini Mungu wetu kuwa ni Mungu wa uweza anaweza, tusiingiwe na hofu tukasahamu kwamba watu tuliookoka tuna thamani kubwa na tuna uwezo mkubwa wa kutamka jambo na kufanya jambo na likafanyika,"amesema Habakuki.
Mwalimu wa theolojia kutoka chuo cha Calvary Mkoani Arusha Habakuki Siroko
akihubiri neno la Mungu katika kanisa la Philadelphia Miracle Temple Ndembezi
Mwalimu wa theolojia kutoka chuo cha Calvary Mkoani Arusha Habakuki Siroko
akihubiri neno la Mungu katika kanisa la Philadelphia Miracle Temple Ndembezi
Askofu wa kanisa la Philadelphia Miracle Temple Baraka Laizer akizungumza na waumini wa kanisa la Philadelphia Miracle Temple ambapo aliwataka waendelee kumwamini Mungu wasikate tamaa wasonge mbele
Askofu wa kanisa la Philadelphia Miracle Temple Baraka Laizer katikati akiwa ma mchungaji Evaline Msangi na Mchungaji msaidizi wa Hanania Clement wakisikiliza neno la Mungu
Baadhi ya wazee wa kanisa la Philadelphia Miracle Temple wakisikiliza neno la Mungu
Mwalimu wa theolojia kutoka chuo cha Calvary Mkoani Arusha Habakuki Siroko baada ya neno la Mungu akiomba pamoja na waumini  wa kanisa la Philadelphia Miracle Temple Ndembezi
Waumini wa kanisa la Philadelphia wakijisndaa kumwabudu Mungu
Waumini wa kanisa la Philadelphia wakiomba
Waumini wa kanisa Philadelphia wakisikiliza neno la Mungu
Waumini wa kanisa la Philadelphia wakiomba
Maombi yakiendelea kwa watumishi wa Mungu
Maombi yakiendelea kwa watumishi wa Mungu

































































Post a Comment

0 Comments