MADIWANI KISHAPU WAIOMBA SERIKALI KUKARABATI BARABARA ZILIZOHARIBIWA NA MVUA

Mwenyekiti wa halmashauri ya eilaya ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye baraza la madiwani

Suzy Butondo,Shinyanga press blog

Madiwani wa halmashuri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuharakisha kukarabati miundo mbinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua za msimu uliopita kwakuwa maeneo mengi bado hayapitiki hali ambayo imepelekea usumbufu mkubwa kwa wananchi wilayani humo.

Hayo wameyasema kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo la robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuwasilisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata zote wilayani humo.

Madiwani hao akiwemo diwani wa kata ya Mwamalasa Bushi Mpina amesema Barabara za kwenye kata yake ni mbovu ijapo kuwa seriksli ilizilifanyiwa ukarabati, lakini baada ya kunyesha mvua zimeharibika sana, hivyo serikali iliangalie suala hilo ili waweze kutengeneza miundombinu ya barabara hizo.

"Tunaishukuru serikali yetu inayoongozwa na mama Yetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na mbunge wetu shupavu Bioniface Butondo kwa kutuletea fedha nyingi kwa ajili ya kufanya maendeleo mbalimbali katika halmashauri yetu,hivyo tunaomba tena itusaidie tuweze kutengenezewa barabara zetu ili ziweze kupitika kiurahisi,"amesema James Kamuga Diwani wa kata ya Igaga.

Kaimu meneja wa wakala wa barabara za vijjini na mijini (TARURA) Joseph Bahati amesema serikali inaendelea na mchakato wa utengenezaji wa barabara zote ambazo zimeharibika katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 huku akianisha barababara zote zenye changamoto.

"Tayari tulifanya utaratibu na mkadarasi yupo katika barabara ya kata ya Mwamashela Negezi na Mwadui Lohumbo tunae mkandarasi lakini tunachangamoto ya mfumo, hivyo mfumo ukirudi barabara hizo zitaendelea kutebgenezwa,"amesema Bahati.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza katika baraza hilo amewataka TARURA kuwapa kazi za ukarabati wa miundombinu ya barabra wakandarasi wenye uwezo, kwani barabara nyingi utengenezaji wake umesimama, kufuatia wakandarasi kukosa mitaji, kwani hawako vizuri kiuchumi.

"Katika kazi hizi lazima tuwe makini na hawa makandarasi ambao hawana mitaji, na wengine wana uwezo mdogo ndiyo maana tunaona hawaendelei kufanya kazi baada ya mfumo kusimama na wao wamesimamisha kazi haziendelei kufanyika kwa sababu hawana mitaji, hivyo niwatake tuwe makini sana ili kuhakikisga kazi zetu zinafanyika kwa wakati"amesisitiza Butondo.

"Pia tunamshukuru Rais wetu mama Samia kwa kuendelea kutupa fedha kwa ajili ya kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo, mama huyu ni shupavu toka aingie madarakani hakuna kazi iliyosimama kila kona miradi ipo hivyo tuendelee kumuunga mkono kwa kazi kubwa anazozifanya"ameongeza Butondo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema tatizo la barabara bado lipo linaendelea kutokana na mvua zilizonyesha, hivyo Tarura lisimamieni suala hili ili wananchi wasiendelee kupats shida jinsi ya kupita kwenda eneo jingine.

"Kwanza nampongeza mbunge waj imbo letu Boniface Butondo amepambana na bajeti imeshapitishwa Bilioni 2.6 nje ya bajeti ya kawaida ya kila mwaka hii itasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za miundombinu ya barabara, tuendelee kumpa ushirikiano ili aendelee kuipambania Kishapu yetu, kwani toka aingie madarakani kuna mabadiliko makubwa yamefanyika"amesema Mkude.

"Kwa kweli Mbunge amekuwa mzungumzaji mkubwa anapokuwa bungeni tunamuona na kumsikia, anapigania Umeme, maji,barabara na mahitaji mengine hivyo tuendelee kumuunga mkono ili alete mabadiliko makubwa katika wilaya yetu ya Kishapu na pia tumpongeze Rais wetu kwa kuendelea kutujari siku kwa siku"ameongeza.

Aidha Mkude amewaelekeza madiwa kwamba wana miezi michache wastaafu, hivyo waendelee kutunza kumbukumbu za vifaa mbalimbali vya halmashauri yakiwemo magari wajue kuna magari mangapi yanayofanya kazi na ambayo hayafanyi kazi ili yasije kufanyiwa hujuma na wataalamu.

Aidha Mkuu wa wilaya huyo amewaagiza madiwani wakawahamasishe wananchi wajiandikishe kwenye daftari la kudumu ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali zamitaa,kila mmoja kuabzia umri wa miaka 18 ana haki ya kujiandikisha.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya ambaye pia ni diwani wa kata ya Mondo amesema karibia barabara zote zinashida hivyo ni vizuri Tarura wakalifanyia kazi ili kero hizi zisiendelee kuzungumziwa.

"Niwaombe tu madiwani wenzangu tukasimamie kikamilifu miradi yetu mbalimbali ili kuhakikisha inakuwa ya kiwango na tukawasisitize wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye ugeni wa uhuru wa mbio za Mwenge katika wilaya yetu,niwaombe tuendelee kushirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo "amesemaJijimya.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Emmanuel Johnson amesemayeye na timu yake ya wataalamu wataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma zao,na watajisimamia wenyewe na kuhakikisha kila mkuu wa idara ana miliki idara yake kikamilifu.

"Niwaahidi tu waheshimiwa kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma zetu na niwatake wataalamu wote tufike mahali tujisimamie wenyewe kila mkuu wa idara amiliki idara yake kama kuna jambo limeshindikana lilete kwangu ili tulitatue,hatutaki mwananchi apate shida ili hata tukihama waseme hapa alikuwa furaniamefanya haya yaliyo mazuri"amesema Johnson.

"Pia tunamshukuru mkuu wa wilaya Joseph Mkude kwa kuendelea kutuunganish kuwa pamoja na kutujengea uwezo,na tumpongeze mbunge Boniface Butondo kwa kuendelea kufanya kazi ya kuleta maendeleo, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, sasa hivi tuna miradi kila kona na miradi hii inajendeka tu,hongera kwa kazikubwa,"amepongeza Johnson.

Aidha katika baraza hilo madiwani wamesema changamoto mbalimbali zikiwemo za huduma za afya elimu na maji,ambapo pia ulifanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye alichaguliwa Manyanda aliyeshinda kwa kura zote 40 ambapi wapiga kura walikuwa 40 hakuna kura iliyoharibika au ya hapana
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonathan akizungumza kwenye baraza la madiwani
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonathan akizungumza kwenye baraza la madiwani
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye baraza la madiwani Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye baraza la madiwani Kishapu

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza kwenye baraza la Madiwani Kishapu
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza kwenye baraza la Madiwani Kishapu
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza kwenye baraza la Madiwani Kishapu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kishspu Shija Ntelezu akizungumza
Mwenyekiti wa halmashauri ya eilaya ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye baraza la madiwani
Diwani wa kata ya Talaga Richard Dominick akizungumza kwenye baraza
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu Frances Manyanda akiwashukuru madiwani kwa kumchagua
Diwani wa kata ya seke Bugoro Frednand Mpogomi akizungumza kwenye baraza la madiwani
Diwani wa kata ya Maganzo Mbalu Jidiga akizungumza kwenye baraza la madiwani


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464