Header Ads Widget

TUME HURU YA UCHAGUZI HAIKUJIANDA, POLISI WACHUNGUZE MATUKIO YA UTEKAJI-"CHADEMA"

TUME HURU YA UCHAGUZI HAIKUJIANDA, POLISI WACHUNGUZE MATUKIO YA UTEKAJI-"CHADEMA"




NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA 

Imeelezwa kuwa  tume ya Taifa ya uchaguzi haikufanya jitihada za ziada kwa ajili ya kuhamasisha wananchi ili kujitokeza kwa wingi katika kuhakiki kujiandikisha na kufanya  maboresho katika daftari la kudumu la mpiga kura hali iliyopelekea mwamko mdogo wa wananchi kujitokeza katika zoezi hilo.

Hayo yameelezwa  Agosti 29,2024 na  katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake ambapo ameiomba tume hiyo  kuongeza zaidi muda wa uandikishaji na uhakiki wa daftari hilo ili wananchi wengi zaidi wapate fursa za kuingiza taarifa zao katika daftari hilo na hatimaye waweze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Tulibaini hali ya mwamko mdogo wa watu kujitokeza katika zoezi hilo katika siku ya tarehe 27 mwezi Agosti mwaka huu ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho ambapo changamoto hiyo imesababishwa na tume huru ya uchaguzi kutokuchukua hatua za ziada katika kuwahamasisha wananchi juu ushiriki wa zoezi hilo”amesema Mnyawami

Katika hatua nyingine, Mnyamwami  pia amezitaka mamlaka zinazohusika na usalama wa raia kufanya uchunguzi wa kina kuhuisian na masuala ya upotevu na utekaji wa wananchi unaoendelea katika baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo mkoa wa Simiyu ili kubaini kwa kina nani wanahusika na matukio hayo na kuwachukulia hatua za kisheria

“Tunatoa wito  kwa jeshi la polisi mkoani Simiyu kufanya uchunguzi wa kina juu ya matukio ya watu kutekwa na kupotea ili kubaini chanzo cha tatizo ni nini hali inayopelekea wananchi kuwa na taharuki na kuishi kwa hofu “ameongeza Mnyawami.

Chadema kanda ya Serengeti ni moja wa wapo ya kanda maalumu iliyoundwa na chama hicho ikiwa ni utekelezaji wa sera ya chama hicho ya kuweka mifumo ya utawala kwa majimbo ili kurahisisha shughuli za utawala  ambapo kanda hiyo inajumuisha mikoa  ya  Shinyanga Simiyu na Mara

 

 

 

Post a Comment

0 Comments