Ifahamike kuwa MH.DK SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa awamu ya sita aliingia madarakani 2021 kwa mujibu wa wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 37 ibara ndogo ya 5 ambayo inabainisha kuwa ikitokea Rais aliyepo madarakani akiaga dunia makamu wake huapishwa kuwa Rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama;
Pia hata utaratibu wa CCM Rais akiapishwa pia utaratibu hufanyika ili kumkabidhi nafasi ya uwenyekiti wa CCM Taifa hivyo Rais Samia mara tu baada ya kuapishwa uliitishwa mkutano mkuu na akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM taifa.
Kimsingi huu wakati ulikuwa mgumu sana kwa taifa letu kuondokewa na Rais aliyepo madarakani nchi na wana nchi tuligubikwa na majonzi na huzuni kubwa baada ya kuodokewa na aliye kuwa Rais DK JOHN MAGUFULI Tukirejea hotuba ya kwanza Mh. Rais DK SAMIA alisema na nukuu
“Leo nimelemewa na kidonda kikubwa moyoni mwangu na mzigo mzito mabegani mwangu”.
Hii ina akisi namna gani sote kama taifa tulikuwa kwenye majonzi na huzuni kubwa isiyo na kifani nahii sio kwa ngazi ya Taifa bali hata katika familia zetu ikitokea kuondokewa na mpendwa hujawa na huzuni na majonzi ,hivyo tulipitia kipindi kigumu na chenye majaribu makubwa sana na nijambo la kumshukuru Mungu tulivuka salama katika hali ya umoja na mshikamano wa taifa letu.
KAZI NA MAJUKUMU YA KWANZA YA RAIS SAMIA
Kwa kuzingatia mazingira ya dharura ambayo MH.Dk SAMIA MSULUHU HASSAN. Akiapishwa kuwa Rais na mkuu wa nchi alikuwa na majuku ya awail ya fuatayyo.
Kuwaondolea hofu wa Tanzania. Hili kimsingi lilikuwa jukumu kubwa la kwanza kama mkuu wa nchi kwa kuwa wananchi walikuwa na mawazo mseto na hili alifanya kwa ufasaha mkubwa kweye somo la urai tunajifunza kuwa kazi ya Rais ni mfariji mkuu wa nchi.
Mfano .kupitia salamu aliyo iasisi kuwa “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wote itikieni kazi iendelee” .Hii salamu ya kifalsafa iliakisi na kuwaondolea hofu wananchi na ilitupatia matumaini kuwa kila jambo linalo fanyika na serikali liko katika mifumo ya kitaasisi na sio mtuu, hivyo wa Tanzania wote tulipata ahueni kuwa nchi iko imara na huu ni uthibitisho kuwa CCM iko imara na mathubuti.
Kazi ieendelee imeonekana katika kuimarika kwa Muungano wetu kama ulivyoasisiwa mwaka 1964 Pia hata katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikendeelea kushika kasi mfano reli ya kikasasa SGR DSM hadi DODOMA imeanza kazi, mraadi mkubwa wa umeme wa nyerere ufiji (NHEP) unaendelea,pia uendelezwaji wa mji wa serikali Mtuma Dodoma unaendelea na hata Ikulu ya Chamwino pia imemalizika kujengwa. Haya ni kwa uchache tu hivyo watanzania hatuna budi. kumuunga mkono Rais samia pamoja na CCM kwa ujumla.
Kuwaunganisha wa Tanzania hapa ndipo tunapoona mantiki ya R4. Hasa ile dhana ya maridhiano. (reconciliation) kwa kuzingatia kuwa nyenzo kuu ya maendeleo ni umoja na mshikamano kama taifa tuwe kitu kimoja kulijenga, Amani ikitawala inahuisha ari ya kazi na uzalishaji wa kiuchumi katika taifa,hivyo dhana ya maridhiano na upatanisho imekuwa nguzo kubwa ya kudumisha upendo na uzalendo wa nchi na pia heshima ya binadamu, ikumbukwe kuwa katika medali za siasa hapo awali kulikuwepo na zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katika kunadi sera na falsafa ya vyama na vyombo vya habari kuhisi kuto tendewa haki ya kuandika habari kwa uhuru kama ilivyo sheria mara tu baada ya kuapishwa aliweza ruhusu shughuLi hizo zote kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii ili ashiria kwamba Rais analenga kuwaunganisha waTanzania wawe kitu kimoja (mshikamano) ili kuleta maeendeleo. pia aliwaachia waliokuwa magerezani wale wenye kesi zenye mnasaba na siasa na pia kuwaita viongozi wa vyama vya siasa kufanya nao mazungumzo ambayo hatimaye hii imepelekea taifa kuwa na utulivu mkubwaa hapa tuna kila sababu ya kumpongeza MH.RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.
Kuimarisha diplomasia ya kikanda na dunia kwa ujumla na hususani diplomasia ya kiuchumi kwa mujibu wa sera ya mambo ya nje (Tanzania foreign policy) ya nchi yetu iliyo nzishwa mnamo 2001 ikichukua taswira ya kuimarisha diplomasia ya uchumi hususani kuvutia wawekezaji na technolojia na utalii ikiwemo utalii wa mikutano na matibabu katika hospital ya Taifa Muhimbili na Benjamini mkapa Dodoma.
Kwa hili tumeshuhudia mwaka 2019/2021 dunia ikiwa kwenye changamoto ya UVICO 19 janga hili lili ifanya dunia kuwa katika mtanziko mkubwa wa diplomaisia kwa mataifa mengi kufunga mipaka na kusitisha safari za ndege na hata wale amabo hawakuapata chanjo ya uviko kuto ruhusiwa kuingia baadhi ya mataifa ila kwa kutambua umuhimu wa kufungua nnchi toka katika huo mtanziko kwa kuruhusu chanjo ya UVIKO 19 hili liliashiria dhamira ya serikali kuhakikisha nchi ina ungana na dunia katika wajibu wa kujilinda dhidi ya majanga yenye mmnasaba wa magonjwa na sio kujitenga kama kisiwaa.na kwa hili hatuna budi kumpongeza Rais samia kwa kuwa kiongozi mwenye kujari na kuthamini Afya za binadamu na wanachi wake kwa ujumla.
Kujali haki za binadamu na utu wa mtu.hiiime dhihirika pale alipo ruhusu ma binti wanapo tokea kushika ujauzito na kujifungua kIsha warejee kwenye mfumo rasmi wa masomo hili ni jambo kubwa lililoonyesha dhamira ya kweli ya mkuu wa nchi kujari utu wa mtuu na heshima yake.hili lime fungua njia kwa mabinti kueendelea na elimu yao vizuri pia tumeona Ujenzi wa shule maalum kwa masomo ya sayansi kwa wasichana mfano Manyara girls.
TUZIFAHAMU 4R ZA RAIS SAMIA NA TIJA YAKE KWA UMOJA WA KITAIFA
1.MARIDHIANO (RECONCILIATION) hii ni kwamba sisi wa Tanzania tuweze kuishi na kudumisha tunu ya Amani,umoja na mshikamano kwa kuzingatia msingi ya maridhiano kwa jambo au mitazamo mseto inapotokea. Na hii si kwa taifa bali hata ngazi ya familia tukijenga desturi ya maridhiano tuta kuwa na umoja na mshikamano na hatimaye upendo miongoni mwetu nahii itapunguza migogoro ya ndoa hata taraka kupungua ,hivyo falsafa ya maridhiano isibaki tu katika medali za siasa na vyama vya siasa bali tuiishi kwa vitendo katika jamii zetu. mfano tumeshuhudia CCM mkoani Mwanza wakichanga fedha kwa ajili ya kumsaidia ndg Tundu Lissu aweze kutengeneza gari yake hii imedhihirisha kuwa kukinzana kimtazamo katika siasa hakuna madhara ya kushindwa kusaidiana katika mambo ya kijamii hili ni jambo la kupongezwaa na limedhihirisha kuwa CCM Kama taasisis ina iishi dhana ya maridhiano Na hii ndio siasa safi aliyo tu husia Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba ili taifa lolote lipate maendeleo linahitaji siasa safi na uongozi bora hivyo CCM imedhihirisha ina ishi kwenye msingi ya siasa safi.
2.USTAHIMILIVI ( RECILIANT) Huu ni msingi wa demokrasia kuvumiliana pale una pokosolewa na hii inasaidia kujenga taifa la watu wenye umoja na mshikamano. Mfano hai tumeshuhudia kiongozi mkuu wa nchi kubaki katika hali ya utulivu na hatimaye hutoa majawabu yasiyo ksi jazba wala kinyongo kwa wanao mkosoa.hii ina tuu fundisha kuwa ustahimilivu nunguzo muhimu sana katika siasa na jamii kwa ujumla.
Mfano 2023 tum shuhudia ukosoaji mkubwa kuhusu mkataba wa bandari na DPW kuhusu uwekezaji, hata taasisis nyingine zika diliki ku msimamo wa kupinga lakini Mh.Rais SAMIA. Alibaki kuwa mtulivu kwa kuwa ana fahamu tija na mantiki ya uwekezaji huu wa kimkakati kwa taifa letu.hii ime ashiria kuwa Rais samia ana ishi katika falsafa ya ustahimilivu na huu ni uthibitisho tosha unao onyesha kuwa ni kiongozi anayefanya siasa safi.
Kwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi amethibitisha kuwa ustahimilivu ni nyenzo nzuri ya kuongoza na kuishi na jamii nasi pia tuiishi hio zana ya ustahimilivu.
Sasa hata katika familia zetu tuwe wavumilivu pale tunapopata changamoto ya kukosolewa hata tuwe tayari kusamehe.hii kwa ufupi tunaita political tolerance.
3.MAGEUZI AU MABADILIKO.-(REFORMS). Hii dhana ina tuhimiza tuwe watu wa mabadiliko na tuwe tayari kwamabadiliko. Hata historia ina tuonyesha kuwa mwaka 1991 kwenye tume ya nyarari ili kuja na maoni ya wananchi juu ya mfumo wa chama kimoja maoni ya wananchi 21% walitaka mfumo wa vyama vingi na 79% litaka mfumo wa chama kimoja ueendelee nah ii imethibitisha namna ilivyo kuwa vigumu watu kupokea mageuzi ya mifumo ila kwa namna Mh Rais Samia anavyo zingatia mageuzi ya mifumo tumeona kuundwa kwa tume mfano tume ya haki jinai. Hii yote ni kuhakikisha mageuzi yana kuwa ya kimifumo kwa mstabali wa taifa.
Nasi watumishi hatuna budi katika maeeneo yetu kuwa na uthubutu wa kufanya mageuzi kwal dhummuni la kuishi hi falsafa ya mageuzi.
4.KUJENGA UPYA.(RE BULD).Hii falsafa ina tuasa kujenga upya pale ambapo pana changamoto ili tuweze kwenda mbele kama taifa.mfano tumeona mabadiliko ya sharia ya uchaguzi. T toka kuwa tume ya Taifa ya uchaguzina kuwa Tume Huru ya uchaguzi. Hii ni matokeo chanya ya hii falsafa ya kujenga upya.
HITIMISHO
Kimsingi Taifa letu lime kirimiwa kuwa na viongozi wa zalendo na wenye mitazamo ya kifalsafa kulingana na alama za nyakati. Kuanzia kuasisiswa kwa taifa letu 1964 mapaka sasa taifa limeendendelea kuwa imara na mathubuti kwa kuwa viongozi wote wa chama na serikali wamekuwa wa kitoa kipaumbele swala la kusimamia tunu za taifa letu, ikiwemo kueenzi muungano Kulinda amani na umoja wa kitaifa. Hivyo Rais SAMIA amaekuwa mfuasi mahiri wa falsafa ya saiasa safi na uongozi bora hivyo Wa Tanzania Tumuunge mkono kwa kila mmoja wete kutimiza wajibu pale anapo fanyia shughuri,kwa pamoja tuna jenga taifa letu.
MAKALA HII IMEANDKWA NA
JOHN FRANCIS HAULE….0756717987
MKUU WA SOKO KUU LA ARUSHA
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464