WAZEE WAKUMBUSHIA AHADI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUTUNGWA SHERIA YA WAZEE

WAZEE WAKUMBUSHIA AHADI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUTUNGWA SHERIA YA WAZEE

Na Marco Maduhu,KISHAPU
BARAZA la ushauri la wazee wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wamekumbushia ahadi ambayo waliahidi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika siku ya wazee duniani ambayo kitaifa ilifanyika mkoani Mtwara mwaka 2019, kwamba itatungwa sheria ya wazee.

Wazee wamekumbushia ahadi hiyo leo Septemba 9,2024 wakati wakiwasilisha mapendekezo na mahitaji yao kwa mbunge wa jimbo la kishapu Boniphace Butondo, ili ayafanyiwe kazi yaliyondani ya uwezo wake pamoja na mengine kuyawasilisha ngazi za juu.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee wilayani Kishapu Suzana Masebu, akizungumza wakati wa kuwasilisha mapendekezo na mahitaji yao kwa katibu wa mbunge kwa niaba mbunge Boniphace Butondo, amesema wanakumbushia ahadi utungwaji wa sheria ya wazee ambayo waliahidiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipokuwa mgeni Rasmi siku ya wazee duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mtwara.

“Tunahitaji sera ya wazee ya mwaka 2003 ihuishwe na kutungiwa sheria ili iwe na nguvu ya kiutekelezaji kama alivyoahidi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa,”amesema Suzana.
Ametaja mapendekezo mengine,kuwa wazee wanahitaji wawe na Pensheni ya kuwasaidia kila mwezi kwa kiasi chochote cha fedha ili wajikimu, sababu wazee wachache wapo kwenye mfumo rasmi na wengine hawapo kwenye mfumo huo.

Mahitaji mengine ni bima za afya kwa wote ziwe na jicho rafiki kwa wazee, sheria mahususi inayowabana watoto na jamii kuwatunza wazee ili kuepuka vitendo vya utekelezaji, kushirikishwa kwenye vikao vya maamuzi yakiwamo mabaraza ya madiwani, suala la kikokotoo lisiwatizame wastaafu tu wa sasa,bali watizamwe na wazamani.
Mapendekezo mengine ni uwepo na mkakati mahususi wa afya kwa ajili ya wazee, kukabiliana na magonjwa yasiyoambukizwa, utengwaji wa madirisha kwenye huduma za afya, pamoja na uwepo wa kitengo cha mikopo inayojitegemea kwenye idara ya maendeleo ya jamii, ili wazee wenye nguvu wapate mikopo hiyo na kuzalisha mali.

Afisa ufuatiliaji masuala ya wazee kutoka baraza la ushauri la wazee mkoa wa shinyanga Laurent Mihayo, amesema kwamba wanakutana na wabunge wote wa mkoa huo,kuwasilisha mapendekezo na mahitaji ya wazee kwa kila halmashauri, ili wayafanyie kazi na kuyawasilisha ngazi za juu kwa kutumia nafasi zao za ubunge.
Katibu wa mbunge wa jimbo la Kishapu Godfrey Mbussa, akizungumza kwa niaba ya mbunge wa jimbo hilo Boniphace Butondo, amesema mapendekezo na mahitaji hayo yamefika sehemu husika, sababu mbunge ni mwakilishi wa wananchi na atayafanyika kazi, na kwamba anafahamu ugeni wa wao lakini amepata dharura yupo kwenye ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara John Mongella ambaye yupo wilayani humo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee wilayani Kishapu Suzana Masebu akisoma mapendekezo na mahitaji ya wazee wilayani humo.
Afisa ufuatiliaji masuala ya wazee kutoka baraza la ushauri la wazee mkoa wa shinyanga Laurent Mihayo akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa mbunge wa jimbo la Kishapu Godfrey Mbussa akizungumza na wazee.
Katibu wa mbunge wa jimbo la Kishapu Godfrey Mbussa
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464