SHYCOM ALUMNI MARATHON 2024 KUTIKISA SHINYANGA SEPTEMBA 21,RC MACHA AJISAJILI KUSHIRIKI MBIO HIZO


SHYCOM ALUMNI MARATHON 2024 KUTIKISA SHINYANGA SEPTEMBA 21, RC MACHA AJISAJILI KUSHIRIKI MBIO HIZO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBIO za Shycom Alumni Marathon 2024 zinatarajiwa kufanyika septemba 21 mwaka huu, katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga,huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akipongeza mbio hizo pamoja na yeye kujisajili ili kushiriki.

Mbio hizo zitakimbiwa umbali wa kilomita 5,10 na 21 ambazo zimeandaliwa na umoja wa watu ambao waliosoma katika Chuo cha Ualimu SHYCOM, kwa lengo la kuchangisha fedha ili kukarabati miundombinu ya chuo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Septemba 14,2024, amesema kuanzishwa kwa mbio hizo za Shycom Alumn Marathon ni jambo jema,sababu fedha zitakazopatikana zitakarabati chuo hicho ambacho kina cha muda mrefu tangu mwaka 1965.

“Nawapongeza sana kwa kuanzisha mbio hizi za Shycom Alumn Marathon na mimi nitashiriki mbio hizi na tayari nimeshajisajili na nimelipia pesa, na mimeambiwa wananchi zaidi ya elfu moja wanatarajiwa kushiriki,”amesema Macha.
Amesema faida za mbio hizo pia zitaunganisha umoja na mshikamano kwa watu ambao wameshawahi kusoma chuo hicho, kuimarisha afya pamoja na kuibua vipaji na kupata wakimbia riadha.

Aidha, ametoa wito pia kwa watu na viongozi, kwamba katika shule zao walizosoma watafutane na kuungana kwa pamoja, ili wajadili namna ya kukarabati shule ambazo walisoma, kwa kuboresha miundombinu ya shule.
Pia, amesema katika mbio hizo kutakuwa na burudani mbalimbali pamoja na uchangiaji wa damu, na kwamba amewahakikishia usalama watu kutoka mikoa mbalimbali ambao watafika kushiriki.

Mratibu wa mbio hizo Anorld Bweichum, amesema maandalizi yake yameshakamilika kwa asilimia 90, na wananchi ambao watashiriki mbio hizo wanapaswa kulipia kiasi cha fedha sh.35,000 ili kujisajili na mgeni Rasmi siku hiyo atakuwa Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda.
Naye mmoja wa ambao wamewahi kusoma katika chuo hicho Robert Kazinza, amesema wameanzisha wazo hilo ili kupata fedha za kuboresha miundombinu ya chuo.

Mwakilishi wa Mkuu wa chuo cha Shycom Shinje Charles, amesema fedha zitazopatikana zitatumia kukarabati mabweni,madarasa, mfumo wa majitaka, na miundombinu mingine ili kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumzia mbio za Shycom Alumni Marathon.
Mratibu wa mbio za Shycom Alumni Marathon Anorld Bweichum akielezea maandalizi ya mbio hizo.
Mwakilishi wa Mkuu wa chuo cha Shycom Shinje Charles akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akijisajili kushiriki mbio hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akionyesha namna alivyojusajili kushiriki mbio hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujisajili ili kushiriki mbio hizo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464