RC MACHA BILIONI 60 ZIMETOLEWA KWA WALENGWA TASAF SHINYANGA,KAYA 9,245 ZIMEHITIMU KWENYE MPANGO BAADA YA KUIMARIKA KIUCHUMI

RC MACHA BILIONI 60 ZIMETOLEWA KWA WALENGWA TASAF SHINYANGA,KAYA 9,245 ZIMEHITIMU KWENYE MPANGO BAADA YA KUIMARIKA KIUCHUMI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amesema katika mkoa huo jumla ya fedha zaidi ya Sh.bilioni 60 zimetolewa kwa walengwa wa TASAF ili kuimarisha uchumi wa Kaya zao.

Amebainisha hayo leo Septemba 27,2024 wakati akifungua kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya za walengwa TASAF111 awamu ya pili.

Amesema shabaha ya serikali katika kutoa fedha hizo za TASAF, ni kuhakikisha kila mwananchi anaishi na kufurahia maisha na rasilimali za nchi, kwa kuimarika kiuchumi.

"Kwa Mkoa wa Shinyanga tangu mwaka 2015 kiasi cha fedha sh.bilioni 60 zimetolewa kwa walengwa wa TASAF ili kuwanusuru na umaskini,"amesema Macha.

Mratibu wa TASAF mkoa wa Shinyanga Dotto Maligisa, amesema katika mkoa huo sasa hivi kuna Walengwa 35,325, na kwamba Walengwa walio ondolewa kwenye mpango baada ya kuhitimu kwa kuimarika kiuchumi ni 9,245.

Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF kutoka makao makuu Haika Shayo, amesema mpango wa TASAF 111awamu ya pili ulianza mwaka 2021 na utaisha Septemba 2025 na ndiyo maana wanafanya tathimini ya mpango huo, na kwamba kwa nchi nzima Walengwa Laki 3 wamehitimu mara baa ya kuimarika kichumi.

Aidha,amewasihi Walengwa ambao wamehitimu kwenye mpango huo, kwamba wasiondoke kwenye vikundi vya Akina na kuwekeza,bali waendelee ili kuendelea kujiimarisha kiuchumi.

Naye Mkuu wa kitengo cha malipo ya kielekitroniki kutoka TASAF Elias Muyomba, ametaja idadi ya Walengwa ambao wanalipwa fedha zao za Ruzuku kwa njia ya mtandao ni 361,592,kwa kutumia simu za mkononi ni asilimia 43 na benki 57 na kuna jumla ya walengwa 79,926,685 na kwamba usajili wa malipo mtandaoni bado unaendelea.

Ametaja takwimu za usajili kwa walengwa wa TASAF kulipwa malipo yai kwa njia ya mtandao mkoani Shinyanga, kwamba Manispaa ya Shinyanga ina asilimia 77,Kishapu 47,Kahama 46,Msalala 30,Ushetu 15 na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga asilimia 9.

"faida ya malipo ya fedha kwa njia ya mtandao,kwanza fedha zao zinakuwa salama,kuzipata haraka,na pia tunapunguza gharama ya kupeleka pesa kwa walengwa, ambapo hatutakuwa na mlolongo wa magari mengi," amesema Muyomba.

Nao baadhi ya Walengwa wa TASAF akiwamo Nyanzobe Madongola na Prisca Shija,wameipongeza Serikali kwa mpango huo, ambao umebadilisha maisha yao kiuchumi,kwa kuboresha makazi,kusomesha watoto hadi chuo kikuu,na kufuga mifugo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni.
Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF kutoka makao makuu Haika Shayo, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa kitengo cha malipo ya kielekitroniki kutoka TASAF Elias Muyomba akielezea malipo ya walengwa wa TASAF kwa njia ya Mtandao.
Mratibu wa TASAF mkoa wa Shinyanga Dotto Maligisa, akiwasilisha taarifa ya TASAF Mkoa wa Shinyanga.
Kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya za walengwa wa TASAF kikiendelea mkoani Shinyanga.
Walengwa wa TASAF wakitoa ushuhuda namna walivyoondokana na umaskini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464