Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Chibe, imedaiwa kubakwa na Juma Mussa Mmhela anayekadiriwa kuwa na umri wa Miaka 45, mkazi wa kijiji cha Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Tukio hilo linasadikika kutokea Ijumaa, tarehe 16 Agosti, majira ya saa kumi jioni, wakati binti huyo alipokuwa akienda kisimani kuchota maji.
Watoto hao waliporejea majumbani mwao walishindwa kujizuia na kuanza kutoa taarifa kwa familia zao, ingawa mwathirika mwenyewe alikuwa bado anashindwa kuzungumzia tukio hilo hata hivyo, baada ya wazazi wa watoto wengine kupata taarifa hizo, walimtaarifu Shangazi yake ambaye alichukua hatua ya kuzungumza na mtoto huyo.
Tulikaa kikao nikamwita mtoto akaeleza kweli alimtaja huyo baba, baada ya hapo yule baba akasemaje sasa wewe mama unasema nikamwambia mimi nahitaji huyu binti akapimwe akawa anakataa badae akaniambia twende tukapime kwenye zahanati za watu binafsi lakini pia aliniambia nimsamehe kwamba hatarudia tena alisema anipe laki tatu yaishe nilikataa badae nikamwambia twende kwenye vipimo tukaenda mimi nikawa nawasiliana na polisi wakati tunaendelea na vipimo kwenye hospitali binafsi polisi walikuja kumkamata tukaenda naye kwenye kituo.
Aidha, ameiomba serikali ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.
Mwenyekiti wa mtaa wa Chibe, Bwana Kashinje Misana, amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kulaani vikali kitendo hicho akisema, "Hili ni tukio la kikatili na lisilovumilika watoto wetu wanapaswa kulindwa na jamii, siyo kudhulumiwa."
viongozi wa jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), wakiwemo katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa Bwana Daniel Kapaya, mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Mwarabu Mwimbili, na katibu wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Bi. Husna Maige.
Viongozi hao wa wamelani vikali tukio hilo huku wakihimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya sheria katika kutoa taarifa za matukio ya ukatili.
Viongozi wa jumuiya ya SMAUJATA wakiwa na Mariam Maganga Masabo shangazi wa mtoto huyo, ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Chibe na pia katibu wa Umoja wa Wazazi (UWT) kata ya Chibe.