BROTHERHOOD SURVEY SERVICES YASHIRIKI SIKU YA USAFI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MANISPAA YA SHINYANGA

Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited wakiendelea kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited ya Mkoani Shinyanga inayojihusisha na Uuzaji Viwanja, uchoraji ramani za ujenzi na kusimamia usafi kwa ujumla imeshiriki Siku ya Usafi Duniani kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi Septemba 21,2024 Mkurugenzi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu amesema wameshiriki siku ya Usafi duniani katika hospitali hiyo ili njema ili kutunza mazingira.

“Leo ni siku ya usafi kimataifa, na sisi kama Brotherhood Survey Services Company Limited tumeitumia siku hii kushiriki kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ambayo imeboreshwa sana. Tunaishukuru serikali kwa namna ilivyofanya kazi kubwa kuboresha sekta ya afya hapa, na sisi tumeamua kuwaunga mkono kutoa nguvu kazi lakini pia kujitolea maarifa na ujuzi kwa kidogo ambacho tunacho kuja kufanya usafi ambao wamekuwa wakifanya usafi kila siku nasi tumeona tuwaunge mkono katika siku hii njema ili kutunza mazingira”,amesema Bulugu.

Ameeleza kuwa, wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali hospitalini hapo kwa sababu Kampuni ya Brotherhood Survey Services Co. Ltd licha ya kujihusisha na uuzaji viwanja pia wanajihusisha na usafi wa majengo ya biashara na makazi na kutunza mazingira.

“Mazingira safi ni maisha yetu, mazingira safi ni uhai wetu, mazingira safi ni afya yetu, mazingira safi ni uchumi wetu hivyo kila mmoja wetu ajitafakari namna anavyoweza kuwa na mchango chanya katika kuyaweka mazingira yetu katika hali ya usafi.

 Siku hii ya Usafi Duniani haijabaki kama siku ya kuondoa taka ngumu tu bali ni siku ya kimkakati wa kutokomeza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu”,ameongeza Bulugu. 

Amesema ni lazima mazingira yatunzwe na kuwepo mkakati mzuri wa kuyaendeleza hivyo ni vyema jamii  ikatunza mazingira huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kufanya usafi katika hospitali hiyo badala ya kuiachia serikali pekee.

Kwa upande wake Afisa Afya wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Frank Batista akiongea kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ameishukuru Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Ltd kwa kushiriki kufanya usafi katika hospitali hiyo huku akiwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza  kufika hospitalini hapo kila mwisho wa mwezi au muda wowote.

Wasiliana na Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited kwa simu 0677000026 au 0677000028 au fika ofisini  Shinyanga Jengo la NSSSF Mpya - Barabara kuu ya Mwanza Ghorofa Na 1.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu akielezea namna walivyoshiriki siku ya Usafi duniani kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Septemba 21,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu akielezea namna walivyoshiriki siku ya Usafi duniani kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Septemba 21,2024 
Afisa Afya wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Frank Batista akielezea umuhimu wa usafi kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu  (kulia) akishiriki kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 

Mfanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited akiendelea kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 

Afisa Afya wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Frank Batista (kushoto) na Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited wakiendelea kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 
Afisa Afya wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Frank Batista (kulia) na Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited wakiendelea kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 
Afisa Afya wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Frank Batista (kushoto) Mkurugenzi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu wakipanda mti katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu akipanda mti katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 
Afisa Afya wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Frank Batista akipanda mti katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga 
Zoezi la kupanda miti katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea

Zoezi la kupanda miti katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464