Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wananchi katika kata ya Bupigi jimbo laKishapu
Suzy Butondo Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo amewaomba wananchi wa jimbo la Kishapu kujitokeza kwa wingi katika kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ifikapo 27 Novemba mwaka huu.
Ombi hilo amelitoa leo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Bupigi na Mwataka alipokuwa kwenye ziara zake za kuhamasisha wananchi wajitokeze wote katika kuchagua viongozi katika uchaguzi wa mitaa ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Kishapu ambapo alitembelea kata ya Bupigi na kata ya Mwataga wilayani Kishapu.
Butondo amesema kila mmoja ana haki ya kuchagua kiongozi, hivyo ni vizuri watu wote wakajitokeza ili kuchagua kiongozi mwenye sifa ya kuongoza anaekubalika kwa wananchi wote,kama watakuwa wanafaa waliokuwa wenyeviti wachaguliwe, kama hakufanya vizuri wachague mwenye sifa.
"Niwaombe wananchi wote wa Kishapu tujitokeze kwa wingi na tuwahamasishe wananchi wote ili siku ile ikifika tutoke bila kusahau wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee tuwasaidie siku hiyo wafike mapema na wapige kura, kwani ni haki ya kila mtu"amesema Butondo.
"Pia niwaombe wanachama wote wa chama cha mapinduzi CCM ambao bado hamjasajiliwa mjisajili ili tuweze kujua idadi yetu ya wapiga kura, niwaombe viongozi wangu mhakikishe kila mmoja amesajiliwa,ameongeza Butondo
Aidha wananchi wa Bupigi na Mwataga wamemshukuru mbunge Butondo kwa kutekeleza ahadi zake zote alizoahidi wakati akiomba kura, hivyo wameomba nyongeza na kuweza kutatua zile kero mbalimbali zilizobaki ijapokuwa asilimia 99 ya maendeleo ametekeleza kwa kushirikiana na Rais Samia Suluhu.
Baadhi ya wananchi hao akiwemo Cheo Kashinje ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Butungwa kata ya Bupigi amesema wanamshukuru mbunge kwa kutimiza ahadi zote alizoahidi wakati akiomba kura, wameamini kwamba Mungu aliwapa kiongozi bora.
"Katika kata ya Bupigi tulikuwa hatuna barabara kabisa lakini baada ya kuingia madarakani miaka minne tu tumepata barabara wananchi walikuwa wakipata shida wakati wakati wa kusafiri kwenda kijiji kingine ama anapopatikana mgonjwa anatakiwa kuwahishwa hospitali lakini sasa barabara zinapitika tunaenda mnada wa mhunze kwa. bei ndogo tu 4000 kwenda na kurudi tofauti na awali unaweza ukatumia 10,000"amesema Kashinje
"Kwa kweli hili ni jembe la Kishapu kuna mbunge mmoja alitudanganya tufyeke minyaa alete barabara tulifyeka minyaa yetu akaenda moja kwa moja hata hakututengenezea barabara, lskini Butondo si muongo ni mbunge mkweli, sijui ulikuwa wapi zamani mbunge wetu machachari"amesema Kashinje.
Aidha Mbunge Butondo alikagua mradi wa maji wenye taki lenye lita100,000 ambapo liwataka Ruwasa wawasogezee mtandao wa maji wananchi ili waweze kusogeza maji majumbani kwani kwa sasa yako mbali wanashindwa kuzimudu gaharama.
Hata hivyo Butondo aligawa mipira na jezi katika timu za vijiji vitatu vya Bupigi ili vijana waweze kucheza kwa sababu michezo ni afya,ambavyo aliwapongeza vijana kwa kujiimarisha kwa michezo
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa katika kata ya Mwataka baada ya kumpokea wananchi
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa katika kata ya Mwataka baada ya kumpokea wananchi
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butndo akizungumza na mwakilishi wa meneja wa Ruwasa Kishapu wakiwa katika mradi wa maji
Diwani wa kata ya Bupigi akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa mbunge Butondo ambapo alimpongeza Mbunge kwa kufanikisha ahadi zote alizoziahidi na kuwaomba wananchi wamuchague tena ili alete maendeleo zaidi na zaidi
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza na wananchi kwenye kikao cha mbunge Mwataga
Mbunge Boniphace Butondo na viongozi wa kata ya Bupigi akikagua jengo la shule ya sekondari la kata ya Bupigi
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa na viongozi wa kata ya Bupigi akikagua mradi wa maji