Header Ads Widget

DOTTO MAGARI AWATAKA CHADEMA KUMSHUKURU RAIS SAMIA 'ACHENI SIASA ZA UONGO'


Na Mwandishi wetu

Dotto Keto, mfanyabiashara maarufu wa magari anayefahamika kama 'Dotto Magari', amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kulinda na kudumisha amani nchini.

Ameisihi CHADEMA kuacha siasa za uongo na badala yake kumshukuru Rais Samia kwa kazi nzuri anayotekeleza kwa manufaa ya taifa.

Magari amesema "Nyinyi majirani zetu mlikuwa hamna ofisi kwa takribani miaka 30, leo Mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa Mikocheni mnataka nini majirani?"

Aidha Magari amewataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Samia kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia, hiyo siyo amani? . Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi”

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama Samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” ,amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments