JUMUIYA YA UMOJA ULAYA & MABALOZI -TANZANIA, WATOA WITO UCHUNGUZI MATUKIO YA UKATILI NA MAUAJI
"Jumuiya ya Umoja wa ulaya kwa makubaliano na mabalozi wa nchi wanachama wa umoja wa ulaya nchini Tanzania,ubalizo wa canada,ubalozi wa Norway,ubalozi wa uswisi na ubalozi wa uingereza,unasikitishwa na taarifa za hivi karibuni za vitendo vya ukatili,kupotea kwa watu na vifo vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu.Tunatoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu matukio haya,Tunatoa pole kwa familia zote zilizoathiriwa.
Tunahimiza serikali ya Tanzania kuhakikisha ulinzi,kama alivyoaahidi Rais.Dr.Samia Suluhu Hassan kupitia mpango wake 4R na kwa mamlaka kuchukua jukumu la kulinda haki za msingi za wananchi,ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza.
Tunakaribisha wito wa Rais wa kuanzisha uchunguzi wa haraka ili kubaini wahalifu waliohusika na kuhakikisha kuna uwajibikaji.
Tunatambua kwa wasiwasi mkubwa kwamba matukio haya ya hivi karibuni yanatishia misingi ya kidemokrasia na haki za wananchi wa Tanzania,katika nchi inayoheshimika kimatifa kwa amani na utulivu na tunaungana na wito wa kulinda amani na utulivu wa nchi"