Header Ads Widget

KATAMBI AWAPONGEZA WALIMU,HUKU AKIWATAKA WAKURUGENZI KUTATUA KERO ZA WALIMU


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi 


Suzy Butondo, Shinysngapress blog

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya katika Taifa la Tanzania la kufundisha watoto misingi ya maisha na maadili mema.

Licha ya kuwapongeza walimu pia amewataka wakurugenzi wote nchini kutatua kero mbalimbali za walimu ili waendelee kufundisha watoto wakiwa na amani.

Hayo ameyasema leo ijumaa 21,2024 wakati akifunga kongamano la walimu wanawake wa chama cha walimu CWT lililofanyika katika manispaa ya Shinyanga na kuhudhuliwa na CWT kutoka mikoa ya Geita, Mwanza, Tabora, Simiyu na Shinyanga, ambapo amesema walimu wanafanya kazi kubwa kwa kuwafundisha watoto misingi ya maisha na maadili mema.

"Kutokana na kazi kubwa wanazozifanya walimu, Rais wetu Samia Suluhu Hassan ametoa agizo la kuwataka wakurugenzi wote tushirikiane kutatua kero za walimu wetu, kama tutashindwa kutatua kero za walimu tujiandae kuachia nafasi, kwani walimu hawawezi kurudi kwenye dhama ya kuuza visheti na sambusa wanatakiwa wawe bize kufundisha wanafunz ili waweze kufsulu vizuri,i"amesema Katambi.

Katambi amesema walimu wanafanya kazi kubwa wanahangaika na watoto, hivyo ni vizuri viongozi wakakumbuka na wao wametoka kufundishwa na walimu mpaka kufikia mafanikio mbalimbali waliyonayo.

"Niwaombe wazazi tuwasaidie walimu wetu kuwafundisha watoto maadili mema, kwani tunawaachia walimu peke yao, sisi wazazi hatuwakemei wanapofanya kinyume na na maadili , tuko bize na maisha tu, hali ambayo imesababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili, tumejisahau kwenda nao makanisani, misikitini na kuzungumza nao kuwaelekeza mema na mabaya, tutawalaumu walimu tu lakini walimu wanahangaika na watoto wetu,"amesema Katambi

"Tuchukueni hatua na sisi wazazi viongozi tufanye majukumu yetu ya kuwalea watoto na kuwafundisha maadili mema, tusiendelee kutoa lawama kwa walimu wetu, tuendelee kuwatia moyo ili waendelee kuipenda kazi yao na kufundisha kwa ubora zaidi"ameongeza.

Aidha akizungumzia kero mbalimbali wanazokutana nazo walimu amesema serikali imetatua kero mbalimbali za walimu na zingine zinaendelea kutatuliwa, na zingine kupandishwa madaraja kupitia vyama vya walimu, na vitengo vingine.

Mnakumbuka Mei mosi ya mwaka 2023 mliwasilisha changamoto zenu za kucheleweshwa kupandishwa madaraja Rais Samia Suluhu aliwaahidi kulishughulikia na mwaka wa fedha 2023/2024 alitekeleza na walipandishwa madaraja walimu 49,540 na mwaka wa 2024/2025 Rais amesema anatarajia kupandisha vyeo walimu 126,353.

"Na katika mwaka 2023/2024 walimu walibadilishwa madaraja 4570 na kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 tinatsrajia kupandisha madaraja kwa walimu 20357, hivyo tunafanya kazi sambamba na viongozi kuhakikisha walimu wanapandishwa vyeo wanapandishwa madaraja, na inatokana na Rais wetu anawapenda walimu ndio maana anaendelea kuwaboreshea na kwenye mapunjo mwaka huu wa fedha mtaona mabadiliko," amesema

"Rais anaendelea kufanya vizuri kazi zake kwa sababu amewekwa kuongoza na Mungu anahakikisha wananchi anawatekelezea mahitaji yao kila sekta anatekeleza, hivyo mama yetu anaendelea kufanya maendeleo makubwa, tuendelee kumuunga mkono watanzania tusiweke nongwa tumpe mauwa yake,"ameongeza Katambi.

Mwenyekiti wa Chama Cha walimu Mkoa wa Shinyanga Mathias John Balele amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuweza kupandisha madaraja mengi kwa walimu, kwani madaraja ni sehemu ya kuongeza mishahara, hivyo Rais ameupiga mwingi.

"Lengo kubwa la kukutana hapa ni kupata elimu na maalifa mbalimbali, juu ya chama chetu na kuanzishwa kwake na kukumbushana malezi ya mamaa mtoto kwa kuamini kwamba kina mama ni jeshi kubwa, na tunamshukuru Rais wetu ameupiga mwingi amekwenda na madaraja mbalimbali yakiwemo ya mseleleko, hivyo tuendelee kumuombea Rais wetu aweze kufanya makubwa zaidi,

"Katika Kongamano hili tumewaalika watu wa kutoka mikoa mingine ikiwa ni pamoja na viongozi wa kitaifa akiwepo Rais wa chama cha walimu Tanzania Reah Ulaya, hivyo niwaombe walimu tuendelee kuiamini serikali yetu kwa sababu tunayo mahitaji mengi ambayo yanatekelezwa,.


"Lakini mengine bado kwa sababu sisi tupo kwenye ajira hayawezi kuisha kwa sababu yanazaliwa kulingana na ajira zinazoendelea kama madai mbalimbali mapya ya mishahara na sasa hivi naibu waziri Katambi ametuahidi wataenda kulipa mapunjo ya walimu na kuajili walimu, hivyo tunaamini tunaenda kuwa na neema kubwa najua kila mtu atakuwa anapanda kwa wakati"amesema Balele


Kwa upande wake Rais wa Chama Cha walimu Tanzania CWT Reah Ulaya amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya kazi kubwa na kuwapandisha madaraja walimu , hivyo wameahidi kufanya kazi kwa weledi mkubwa, na wataendelea kumwamini Rais siku zote, na wanaahidi kufanya kwa vitendo mwakani.

"Tunaomba utufikishie salamu zetu kwa mama yetu mama Samia mwambie tunampenda sisi walimu wa Tanzania tupo nae bega kwa bega atayaona matokeo yetu mwakani,"amesema Ulaya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi akizungumza na walimu wa chama cha CWT  
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi akizungumza na walimu wa chama cha CWT
Rais wa Chama Cha walimu Tanzania CWT Reah Ulaya akizungumza na wanawake wa chama cha CWT
Rais wa Chama Cha walimu Tanzania CWT Reah Ulaya akishukuru jambo


Mwenyekiti wa Chama Cha walimu Mkoa wa Shinyanga Mathias John Balele akifafanua jambo kwa waandishi wa habari

Mwenyekiti wa Chama Cha walimu Mkoa wa Shinyanga Mathias John Balele akiteta jambo na naibu waziri Katambi
Rais wa Chama Cha walimu Tanzania CWT Reah Ulaya akiteta jambo na Naibu Waziri Katambi


Walimu wakisoma risala 



Walimu wakiwa wamembeba katambi baada ya kufurahishwa na nasaha alizozitoa katika kongamano hilo
Walimu wakiwa wamembeba katambi baada ya kufurahishwa na nasaha alizozitoa katika kongamano hilo

Walimu wakicheza pamoja na Naibu waziri baadaya kumaliza kuzungumza nao 

Walimu wakiwa wamembeba katambi baada ya kufurahishwa na nasaha alizozitoa katika kongamano hilo

Burudani ikiendelea kwa walimu na viongozi wote
Naibu waziri Katambi akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga
Walimu wanakwaya wakiwa kwenye picha ya pamoja na naibu waziri Katambi
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wenye ulemavu wa viungo
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu waziri Katambi
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu waziri Katambi
Viongozi wa CWT wakikabidhiana mataili sita ya gari  waliyokabidhiwa na naibu waziri Katambi 

Viongozi wa CWT wakikabidhiana mataili sita ya gari  waliyokabidhiwa na naibu waziri Katambi 

Walimu wakifurahia baadaya Naibu waziri Katambi kusema neno

Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Naibu waziri akizungumza

Baadhi ya madiwani wakimsikiliza Naibu waziri Katambi akizungumza

Baadhi ya madiwani wakimsikiliza Naibu waziri Katambi akizungumza
Baadhi ya madiwani wakimsikiliza Naibu waziri Katambi akizungumza
Baadhi ya madiwani wakimsikiliza Naibu waziri Katambi akizungumza
Baadhi ya madiwani wakimsikiliza Naibu waziri Katambi akizungumza

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akiwa na vingozi wakimsikiliza Naibu waziri Katambi akizungumza
Naibu waziri Katambi akiombewa baada ya kuzungumza na walimu
Naibu waziri Katambi akiombewa baada ya kuzungumza na walimu




Post a Comment

0 Comments