Mwenyekiti wa wanawake na mama Samia mkoa wa Shinyanga Husna Ally akizungumza na wanawake waliohudhuria mkutano wa wanawake na Samia katika kata ya Chamaguha
Suzy Butondo,Shinyanga
Kikundi cha wanawake na Samia Mkoani Shinyanga kimewashauri wanawake mkoani humo kuachana na mikopo ya Kausha damu iliyopo mitaani, ambayo imekuwa ikisababisha wanawake kushindwa kulea watoto na wengine kusababisha kuzikimbia familia zao.
Licha ya kuwapa ushauri huo wamewaomba kuendelea kupinga ukatili wa kijinsia na wa aina mbalimbali na wakiona mtu kafanyiwa ukatili watoe taarifa sehemu husika ikiwemo dawati la jinsia.
Hayo ameyasema leo mwenyekiti wa kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga Husna Ally wakati akizungumza kwenye mkutano na wanawake wa kata ya Chamaguha, ambapo aliwashauri kuendelea kupinga ukatili wa kijinsia na wa aina yoyote.
Husna amesema Wanawake wengi wamekuwa wakijiingiza kwenye mikopo inayoitwa kausha damu au mikopo umiza, ambayo imekuwa ikisababisha wanawake wengi kushindwa kuhudumia familia zao inavyotakiwa, na wakati mwingine kusababisha watoto kuwa watoto wa mitaani.
"Niwaombe sana mama zangu dada zangu tuachane na mikopo ya kausha damu mikopo umiza, ambayo imekuwa ikisababisha wanawake wengi kuwaumiza waume au kuumiza watoto wao kwa kushindwa kuwahudumia pale wanapohitaji huduma, hivyo tuende tukakope kwenye taasisi za serikali, ili tuweze kuwalea watoto wetu na kuwafundisha maadili mema na tuwahudumie waume zetu ipasavyo"amesema Husna.
Kwa upande wake Katibu wa wanawake na Samia Tatu Almas amesema wanawake na mama Samia ni umoja ambao umeanzishwa ukiwa na lengo la kuunga mkono kazi zote zinazofanywa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, kufuatia utekelezaji wake wa ilani ya Chama Cha mapinduzi CCM.
"Na umoja huu unaunganisha wanawake wote ili tuweze kuungana, tutumie vipawa vyetu kuhakikisha tunasapoti kazi kubwa zinazofanywa na Rais wetu mama Samia Suluhu, ambazo zinaonekana,"ameeleza Almas
Almas amesema Umoja huu unasimamia kamati saba, ambazo ni kamati za ya uchumi na uwezeshaji wanawake, kamati ya ukatili wa jinsia na sheria, kamati ya elimu na lishe mashuleni, kamati ya mazingira na usafi, na kamati ya maadili malezi na vijana.
"Katika eneo la malezi kweli wanawake tumelegalega sana, tupo bize kupambana na kausha damu tumesahau kabisa kulea watoto wetu na wengine tumefikia hatua ya kuwakimbia watoto na kuwaachia familia zetu, hali ambayo sasa imekuwa ikisababisha kufanyiwa ukatili wa kubakwa, kwa watoto wetu wa kike na wakiume kulawitiwa, na wengine kuwa watoto wa mitaani tu, niwaombe wanawake wenzangu tuwarudie watoto wetu tuwafundishe maadili mema ya kidini ili tuwe na watoto ambao watatusaidia baadae"amesema Almas
"Tuwasisitize watoto wetu kwenda kanisani, kwenda misikitini ili wakafundishwe maadili mema ya kimungu, lakini tukiwaacha baadae watakuwa maadui zetu na kutufanyia ukatili sisi wazazi kwa sababu hatukuwalea vyema, kila mzazi mungu amsaidie ili aweze kumsaidia mtoto kimalezi, mama Samia anasikitishwa sana kusikia mmomonyoko wa maadili kwa watoto wetu,"ameongeza
Baadhi ya wanawake akiwemo Ryidia Musa wamesema wanamuomba Rais Samia aweze kuwaletea mapema fedha za mikopo zenye riba nafuu ili waweze kuondokana na mikopo umiza, wanashindwa kujitoa kwenye mikopo umiza kwa sababu wamekuwa wakijikuta hawana pa kushika, lakini wakipata fedha hiyo hawataendelea tena na kausha damu
"Ni kweli hatupendi kukaushwa damu ila tunapojikuta tunashida ndiyo maana tunakimbilia huko,lakini kwa vile mama yetu ni mwenye huruma nasisi tunaomba tu awahishe hizi fursa za mikopo ili tuweze kujikwamua wanawake tunaweza na tukiwezeshwa zaidi tunafanya vizuri,"amesema Mariam Kulwa.
Aidha katibu wa wanawake na Samia Tatu aliwahamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kwani wanaweza kama wameweza kulea familia hata kuongoza jamii wanaweza hivyo wajitokeze wasiogope.
"Niwaombe tu wanawake wenzangu mjitokeze katika kugombea uchaguzi unaotarajia kuanza tarehe 27/11/2024 kwani kila mmoja ana haki ya kugombea, hivyo tuhamasishane tuangalie kina mama wenye sifa za kuongoza tuwashauri wagombee na tuwachague,"amesema Tatu.
Mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Shinyanga Husna Ally akisalimia wanawake waliohudhuria mkutano wa wanawake na mama Samia
Mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Shinyanga Husna Ally akizungumza na wanawake waliohudhuria mkutano wa wanawake na mama Samia

Katibu wa wanawake na Samia mkoa wa Shinyanga Tatu Almas akizungumza na wanawake waliohudhuria mkutano wa wanawake na mama Samia

Mwenyekiti msaidizi wa wanawake na Samia Ester Kika akizungumza na wanawake na Samia waliohudhuria katika mkutano wa wanawake na Samia

Viongozi wa wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye mkutano wa wanawake na Samia

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake kata ya chamaguha Mama Maganga akizungumza kwenye kikao cha wanawake na Samia kilichofanyika kata hiyo
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake kata ya chamaguha Mama Maganga akizungumza kwenye kikao cha wanawake na Samia kilichofanyika kata hiyo
Wanawake wa kata ya Chamaguha waliohudhuria katika mkutano wa wanawake na Samia wakimsikiliza mwenyekiti
Wanawake wa kata ya Chamaguha waliohudhuria katika mkutano wa wanawake na Samia wakimsikiliza mwenyekiti
Wanawake wa kata ya Chamaguha wakicheza kabla ya kuanza mkutano ulioandaliwa na viongozi wa wanawake na Samia
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464