Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akikabidhi mipira kwa mwalimu mkuu wa shule ya Bubiki Winifred Kauma
Suzy Butondo, Shinyanga pressblog
Wananchi wa kata ya Bubike jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga wamempongeza mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo kwa kuwapelekea miradi mingi ya maendeleo katika kata yao kwa kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo miradi ya maji, umeme na madarasa.
Pongezi hizo wamezitoa jana kwenye mkutano wake uliofanyika katika kijiji cha Bubike jimbo la Kishapu mkoani hapa, ambapo wamesema toka aingie madarakani ametekeleza miradi mingi ikiwemo miradi miwili ya umeme na miradi ya maji.
Wananchi hao akiwemo Emmanuel Kasomi na Charles Nhambo wamesema kata yao imepewa kipaumbe kikubwa kwa kupelekewa maji na umeme na hizo zote ni juhudi za mbunge, kwani anapokuwa bungeni halali usingizi kazi yake kubwa ni kuwasemea changamoto zilizopo na zinatekelezwa na zingine zinaendelea kutekelezwa.
"Tunakushukuru sana mheshimiwa mbunge wetu Boniface Butondo Ng"wanang"wanza kwa kuendelea kufanya kazi nzuri ya kutuletea maendeleo, kwani toka uingie madarakani ndani ya miaka minne tunaona mabadiliko makubwa na tunakusikia bungeni unaunguruma kweli wewe ni jembe la Kishapu,"amesema Charles Nhambo.
Diwani wa kata ya Bubike James Kasomi amesema anampongeza mbunge Butondo kwa kuwapelekea. miradi mingi ya maendeleo katika kata hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3.5 ambayo bila mbunge miradi hiyo isingekuwepo.
"Kwanza nikushukuru mheshimiwa kwa kuipendelea kata hii kwa kuleta miradi mingi ya kimaendeleo ipo miradi ya maji ambayo ina thamani ya shilingi bilioni 1.2 ambayo ipo katika kata hii kwa maana ya vijiji vyote kati ya vitongoji 16 kuna vitongoji viwili tu ndiyo havina maji, hivyo tunakuomba uviweke kwenye bajeti ili vitongoji hivi vipate maji ambavyo ni vitongojji vya Bubiki na kingine kipo Nyasamba.lakini kwa ujumla kila kijiji kinamaji na wananchi wengi wanavuta maji kwenye miji yao "amesema Diwani Kasomi.
Diwani akizungumzia sula la umeme amesema toka aingie madarakani Butondo amehakikisha ameleta miradi miwili ya umeme ambayo uliileta ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na giza na kweli amefanikiwa wananchi wapo kwenye mwanga wa umeme katika kijiji hiki cha bubike lakini kijiji cha Bubiki B utekelezaji unaendelea na jana Tanesco walikuja hapa kwa juhudi za mbunge Butondo.
"Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita ya Mama yetu Mama Samia kwa kuendelea kushirikiana na mbunge wetu, kwa kweli Bubiki inaongoza kwa miradi mingi, lakini kwa vile mbunge wetu ni mpiganaji tunaamini mapungufu yaliyopo yataisha kwa sababu tunaona juhudi zako za kuleta maendeleo ni kubwa,"amesema Kasomi.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo amesema yeye yupo kwa ajili ya wananchi wa kishapu, na kazi yake kubwa ni kuhakikisha wanapata mahitaji ya kijamii yote, hivyo alimuomba Meneja wa RUWASA Dickson Kamazima aeleze ni lini vitongoji vilivyobaki vitapata maji na maeneo mengine ya Kishapu.
"Meneja wa RUWASA naomba uelezee utekelezaji wa mpango wa haraka na mfupi huu ambao tunao sasa wa kisima kirefu na mpango mwingine wa muda mrefu wa Ziwa Viktoria, kuna watu wakutoka kata ya Mondo Busangwa Seke Bugoro, hivyo naamini hapa wapo wajumbe watapeleka ujumbe, hivyo naomba uje ueleze ili wajue wananchi mpango huu"amesema Butondo.
"Wakati naingia madarakani kata ya Maganzo ndiyo ilikuwa na maji na makao makuu ya Mhunze mpaka sasa kata 12 tumepekeka maji ya ziwa Victoria ambazo ni Igaga, Mwamashele, Lagana, Mwakipoya Ukenyenge,Uchunga Bupigi Songwa Mwataga, ldukilo, Bubike na ndani ya miaka minne tu sasa tuna kata 14 kata zinatumia maji ya Ziwa Victoria, serikali inafanya kazi kubwa"ameongeza.Butondo.
"Naomba niwakumbushe kwamba mradi wa kwanza kabisa maji ya kisima kirefu tumeleta hapa hapa kata hii ya Bubiki baada ya kuona mnapata shida ya maji, baadae tukapeleka Talaga, jijongo Itilima tuna tanki la kusambaza vijiji vitatu kata ya Masanga Shagihilu maji yanatumika, Ndoleleji na Mwamalasa,"ameeleza.
,"Mmi wakati naingia madarakani upatikanaji wa maji ilikuwa asilimia 31 tu, lakini tukikamilisha mwaka huu wa fedha miradi hiyo tutakuwa na asilimia 72 mimi silali kwenye suala la maji na maendeleo ya Kishapu, mimi sio sanamu ni mbunge wa kazi nipo katika kuhakikisha wananchi wangu mnapata mahitaji yenu ,kwa sababu na mimi ni miongoni mwenu naijua shida ya maji kwa sababu ni mkaaji wa Kishapu" amesema
"Mama yetu Rais Samia Suluhu amesema kuwa hitaji namba moja katika nchi yake ni kuhakikisha kwamba anapeleka maji vijijini, na tayari amenunua mitambo ya kuchimba visima virefu, ambapo tumenza na vijiji vitano ambavyo vina changamoto ya maji, amefanya hivyo kwa kuwahurumia wanawake, kwani wanateseka sana kufuata maji umbali wa kilomita kadhaa"ameongeza Butondo.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kishapu Kamazima amesema tayari wana miundombinu ya kutosha wana matanki mawili ya lita laki moja moja, ambayo maji hayo yanatosheleza kabisa, hivyo vitogoji hivyo tutapiga gharama yake ya kufikisha miundo mbinu ili tupeleke maji wamekuwa wakishirikiana sana na mbunge akiwa bungeni anapiga simu kuwa tunaendeleaje
"Kuna kata 13 ambazo zitapitiwa na bomba la maji ya ziwa victoria ikiwemo kata ya Bubiki, kwani tumepeleka maji Kata mbalimbali ikiwemo Lagana Ngofila hadi Kiloleli, hivyo tuwaombe wananchi muwe wavumilivu tu maji ya ziwa Victoria yanakuja,"amesema Kamazima.
Aidha katibu muenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kishapu Jiyenze Selelii amewataka viongozi wa CCM kata wamuache Mbunge wa jimbo afanye kazi zake, wasikubali kushawishiwa na watu ambao wanaokuja kutaka ubunge na kusababisha taharuki,watu hao waache mara moja wasubiri wakati ukifika wataruhusiwa, "lakini kwa sasa ni marufuku kuleta taharuki kwenye chama niwaombe viongozi mtekeleze ilani ya CCM"
Hata hivyo mbunge Boniface Butondo alikabidhi mipira na jezi kwa timu ya shule ya sekondari Bubike kwa timu ya wanawake na timu ya wanaume na timu ya vijana wa Bubiki ili waweze kuendeleza michezo kwani michezo ni afya.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akikabidhi mipira kwa mwalimu mkuu wa shule ya Bubiki Winifred Kauma
Wananchi wa kata ya Bubiki wilaya ya Kishspu wakimsikiliza mbunge Boniface Butondo akizungumza
Wananchi wakicheza na kufurahia na mbunge wao Boniface Butondo
Kazi inaendelea katika kata ya Bubike
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akikabidhi mpira kwa timu ya vijana Bubiki
Diwani wa kata ya Bubiki James Kasomi akizungumza kwenye mkutano wa mbunge uliofanyika katika kata hiyo
Charles Nhambo mkazi wa Bubiki akimpongeza mbunge wa Kishapu kwa kupeleka miradi mingi mingi ya maendeleo katika kata hiyo
Mbunge wa Kishapu Boniface Butondo akisalimiana na wananchi wa kata ya Bubiki na kusikiliza kero zao mmoja mmoja
Mbunge wa Kishapu Boniface Butondo akisalimiana na wananchi wa kata ya Bubiki na kusikiliza kero zao mmoja mmoja
Mbunge wa Kishapu Boniface Butondo akisalimiana na wananchi wa kata ya Bubiki na kusikiliza kero zao mmoja mmoja
Mbunge wa Kishapu Boniface Butondo akisalimiana na wananchi wa kata ya Bubiki na kusikiliza kero zao mmoja mmoja