WANANCHI WA MHUNZE WAMEONYESHA MAHABA YA DHATI KWA MBUNGE BUTONDO
Na Marco Maduhu,KISHAPU
WANANCHI wa Mhunze wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wameonyesha mahaba ya dhati(upendo) kwa Mbunge wao Boniphace Butondo,kutokana na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo na kutatua shida zao.
Wameonyesha mahaba hayo leo Oktoba 7,2024 kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika mji wa Mhunze na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
Butondo akizungumza kwenye mkutano huo,amesema ndani ya miaka yake minne ya ubunge katika jimbo hilo la Kishapu,ametekeleza miradi mingi ya maendeleo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, na kutatua kero za wananchi.
MAJI.
Amesema kipindi anaingia kwenye ubunge mwaka 2020 kata ambazo zilikuwa na maji ya ziwa victoria ni 3 tu, lakini kwa kipindi chake zimefikiwa kata 18 na bado miradi inaendelea kutekelezwa.
"Wananchi ambao tayari mnamaji vuteni majumbani kwenu, lengo la Rais Samia ni kumtua ndoo kichwani mwanamke ndiyo maana anatoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya maji," amesema Butondo.
BARABARA
Amesema miundombinu ya imetekelezwa maeneo mbalimbali na kwamba katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kujenga kilomita 20 za barabara za lami kutoka Kolandoto hadi Mhunze.
AFYA
Amesema serikali imetoa fedha nyingi chini ya Rais Samia na kuboresha huduma za afya ikiwamo hospitali ya wilaya ya Kishapu pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba,madawa na kuajiriwa watumishi wa afya.
"Kipindi naingia kwenye ubunge hospitali ya wilaya ya Kishapu kulikuwa na majengo matano tu, lakini sasa hivi yapo 15 na Rais ametoa tena fedha Sh.milioni 300 kujenga jengo la utawala,"amesema Butondo.
Amesema kutoka na ukosefu wa Zahanati katika kijiji cha Mwasele, amemuagiza diwani wa Kishapu kwamba atafute eneo la ujenzi wa zahanati hiyo na yeye atachangia mifuko 100 ya saruji.
MNADA
Amesema serikali imetoa sh.milioni 760 kwa ajili ya ujenzi wa Mnada mpya wa Mhunze ambao utaimarisha pia huduma ya vyoo, kero ambayo imekuwa ikilalamikiwa ya ukosefu wa huduma bora ya vyoo kwenye Mnada huo.
"Katika jimbo hili la Kishapu nitahakikisha nalibadilisha kimaendeleo chini ya Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan,"amesema Butondo.
DIWANI.
Diwani wa Kishapu Joel Ndetoson, amempongeza Butondo kwa ushirikiano wake katika kutatua changamoto za wananchi chini ya Rais Samia, na kwamba katika Kata hiyo, wameshapokea fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
WANANCHI.
Nao wananchi wa Kishapu, wamesema jimbo hilo kipindi hiki ndiyo limepata Mbunge sahihi ambaye anajua shida za wananchi na wamekuwa wakimuona bunge Dodoma kupitia television namna anavyowasemea matatizo hayo na mengine tayari yameshatatuliwa.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo bado anaendelea na ziara yake jimboni humo kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara ambapo kesho atakuwa katila mji wa Maganzo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Itikadi na uenezi CCM wilaya ya Kishapu Jiyenze Seleli akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Benard Werema akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kishapu Joel Ndetoson akizungumza kwneye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kulia) akifurahia ushirikiano ambao anauonyesha diwani wa Kishapu Joel Ndetoson katika kutatua changamoto za wananchi na kuwaletea maendeleo.
Mkutano ukiendelea.
Awali vijana wa bodaboda wakimpokea Mbunge wao Boniphace Butondo