Header Ads Widget

SHINYANGA WAVUNJA REKODI MAPOKEZI YA KATIBU MKUU CCM BALOZI DK.EMMANUEL NCHIMBI

Shinyanga wavunja rekodi mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi, ameanza ziara leo Oktoba 9,2024 mkoani Shinyanga, kwa kuzungumza na viongozi wa Chama hicho, pamoja na wananchi kwenye mikutano ya hadhara.

Dk. Nchimbi akizungumza wakati wa mapokezi katika Ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema tangu wafanye ziara katika mikoa 18, Mkoa wa Shinyanga wamevunja rekodi kwa mapokezi makubwa.

"Tunashukuru Shinyanga kwa mapokezi ya kishindo,"amesema Dk. Nchimbi.

Naye Katibu wa Itikadi uenezi na mafunzo CCM Taifa Amos Makalla, amesema Shinyanga ni Mkoa wa 19 wamefika kufanya ziara,lakini kwa mapokezi hayo makubwa inaonyesha Shinyanga ni Ngome ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza wakati wa mapokezi Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuanza ziara yake.

Post a Comment

0 Comments