CCM YAHAMASISHA WANANCHI WAJITOKEZE KWA WINGI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MAKAZI KUANZIA LEO OKTOBA 11

CCM yahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha daftari la wakazi

Na Marco Maduhu,KAHAMA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimewahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wakazi, ili siku ya uchaguzi wa Serikali za mitaa novemba 27 wapate fursa ya kupiga kura.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 11,2024 na Katibu wa Itikadi,siasa,uenezi na mafunzo CCM Taifa Amosi Makalla,wakati Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi alipokuwa akisalimiana na wananchi wa Kagongwa Manispaa ya Kahama.

Amesema siku ya kujiandikisha wananchi kwenye datfari la Makati imeanza leo Oktoba 11,na litakwenda hadi tarehe 20,na kuwasihi wananchi kwamba wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili wapate fursa ya kupiga kura Novemba 27.

"Siku ya kujiandikisha kwenye daftari la makazi imeanza leo hadi tarehe 20, hivyo nawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi mkajiandikishe kwenye daftari hilo ili mpate fursa ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wazuri ambao watawaletea maendeleo," amesema Makalla.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi, amesema chama hicho kitawapelekea wananchi wagombea wazuri wasio na makandokando na wenye sifa zote ambao watawaletea maendeleo,na hivyo kuwasihi wasifanye makosa bali wachague wagombea wa CCM.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464