Header Ads Widget

MRADI BOMBA LA MAFUTA GHAFI AFRIKA MASHARIKI EACOP UMEFIKIA ASILIMIA 45 YA UTEKELEZAJI

Mradi wa bomba la mafuta ghafi Afrika Mashariki EACOP umefikia asilimia 45 ya utekelezaji

Na Marco Maduhu,NZEGA

MRADI wa ujenzi wa Bomba la kusafirisha Mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP), kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania,ujenzi wake umefikia asilimia 45.5.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 18,2024 na Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi (EACOP)kutoka Shirika la maendeleo la petrol Tanzania (TPDC) Asiadi Mrutu,wakati wajumbe wa Tume ya kitaifa ya mipango, wakiwa wameambatana na wajumbe wa bodi ya TPDC,walipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha mifumo ya upashwaji jopo mafuta ghafi,kilichopo Kijiji cha Sojo wilayani Nzega mkoani Tabora.

Amesema ujenzi wa bomba la mafuta ghafi EACOP, unaendelea vizuri na kwamba kwa sasa umefikia asilimia 45.5 huku ukitoa ajira kwa wananchi 7,584 na asilimia 99.3 ya wananchi wameshalipwa fidia zao,pamoja na wananchi 294 ambao walipoteza makazi baada ya kupitiwa maeneo yao na mradi huo wameshajengewa nyumba na kukabidhiwa.
Aidha,amesema kwa upande wa ujenzi wa kiwanda hicho cha upashwaji joto mafuta ghafi kilichopo Sojo chenyewe ujenzi wake umefikia asilimia 96 na kilizinduliwa Rasmi na Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati Machi 26,2024.

"Kwa ujumla mradi mzima wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP) kwa Uganda na Tanzania umefikia asilimia 45.5,"amesema Mrutu.
Naibu Katibu Mtendaji Tume ya kitaifa ya mipango anayeshughulikia masuala ya menejimenti na utendaji na tathimini ya miradi ya maendeleo Dk.Linda Ezekiel,ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya ufundi na madeni, amesema wamefurahishwa kuona uwekezaji huo mkubwa mradi wa EACOP ambao ni fursa kwa Watanzania.

Amesema wameamua kutembelea mradu huo wa EACOP ili kuona utekelezaji wake kwa uhalisi na kufurahishwa na kasi ya ujenzi wake na kwamba mwaka 2026 utakamilika na kuanza kutembeza mafuta kutoka Uganda hadi Tanga.
"Ujenzi wa mradi huu una kwenda vizuri, na nimefurahia kuona Jamii husika imeshirikishwa, Watanzania wengi wameajiriwa na unasimamiwa na Watanzania pia,jambo ambalo nila kujivunia na sisi tuna weza kusimamia miradi mikubwa," amesema Dk.Linda.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka TPDC Balozi Msaafu Peter Kallaghe, amesema wameridhika na maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho hapo Sojo, na kwamba wanajivunia mradi huo wa EACOP kusimamiwa na Watanzania na ujenzi wake unaendelea vizuri.

Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki EACOP kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleni Tanga lina urefu wa kilimolita 1443.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka TPDC Balozi Msaafu Peter Kallaghe akizungumza katika ziara hiyo.
ratibu wa Mradi wa bomba la mafuta Ghafi (EACOP)kutoka Shirika la maendeleo la petrol Tanzania (TPDC) akielezea mradi wa EACOP .
Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Madeni Dk.Linda Ezekiel akizungumza katika ziara hiyo.
Kiwanda cha upashaji joto mafuta ghafi kilichopo Kijiji cha Sojo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Wajumbe wakiwa ziara katika Kiwanda cha kuwekwa mifumo ya upashwaji Joto mafuta ghafi kilichopo Sojo wilayani Nzega.
ziara katika Kiwanda cha kuwekwa mifumo ya upashwaji Joto mafuta ghafi kilichopo Sojo wilayani Nzega.

Post a Comment

0 Comments