Header Ads Widget

KUWASA WATEMBELEA CHANZO CHA MAJI YA ZIWA VICTORIA IHELELE,UHARIBIFU WA MAZINGIRA MADAKIO YA MAJI WASHITUA


KUWASA WATEMBELEA CHANZO CHA MAJI YA ZIWA VICTORIA IHELELE,UHARIBIFU WA MAZINGIRA MADAKIO YA MAJI WASHITUA

Na Marco Maduhu,IHELELE

BODI ya Wakurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama(KUWASA)imetembele chanzo cha uzalishaji Maji ya Ziwa Victoria kilichopo Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza,huku ikisikitishwa na uharibifu wa mazingira kwenye madakio ya maji.
Chanzo hicho cha maji kinasimamiwa na kuendeshwa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Kahama-Shinyanga (KASHWASA)ambao huzalisha maji hayo na kuyasambaza kwenye mamlaka za maji,watoa huduma ya maji ngazi ya jamii na kwenye migodi ya madini.

Ziara hiyo imefanyika leo Oktoba 21,2024 ili kuona namna maji yanavyo vunwa na KASHWASA kutoka ndani ya Ziwa Victoria,kutibiwa na hadi kusafirishwa kwenda kwa wateja wake na kuwafikia wananchi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Stewart Bulaya,akizungumza katika ziara hiyo,ameipongeza Serikali kwa uwekezaji huo mkubwa, ambao umeondoa kero ya wananchi wengi ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama.

Ameipongeza KASHWASA kwa kuonyesha uzalendo mkubwa wa kusimamia mradi huo na kuendesha vizuri licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ya kutolipwa bili za maji kwa wakati na Mamlaka za maji ambazo wanaziuzia maji,lakini wamekuwa wakitoa huduma bora.
"Sisi KUWASA hata chanzo kingine cha maji,matumaini yetu yote yapo KASHWASA, hivyo tunaomba mipango yenu mizuri ambayo mmekuwa mkiipanga muitekeleze kwa vitendo,sababu Watanzania wengi wanawategemea sana katika upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama,"amesema Bulaya.

Aidha,amezitahadharishwa mamlaka mpya za maji ambazo zimekuwa zikiuziwa maji na KASHWASA kwamba wasiige tabia ya kulimbikiza madeni,huku akiziomba mamlaka ambazo zinadaiwa walipe madeni yao ili kuiwezesha KASHWASA kuendelea kutoa huduma bora ya maji.
Katika hatua nyingine amezungumzia suala ya uharibifu wa mazingira, kwamba KASHWASA waone uwezekano wa kuweka alama za mipaka kwenye madakio ya maji ili wananchi wasivamie na kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kushirikiana na Ofisi ya makaumu wa Rais mazingira kudhibiti uhalibifu huo wa mazingira.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa KASHWASA John Zengo,ambaye ni Meneja biashara akisoma taarifa, amesema chanzo hicho kilianzishwa mwaka 2003 na kukamilika mwaka 2008 na kuzinduliwa mwaka 2009 na gharama zake ni sh.bilioni 254 ambazo ni kodi za Watanzania.
Amesema chanzo hicho kwa sasa kina zalisha maji lita milioni 72, kwa siku, huku uwezo ni kuzalisha lita milioni 80, na mradi ukipanuliwa una uwezo wa kuzalisha lita milioni 120.

Ametaja changamoto kubwa ambazo zinawakabili,ni kuwapo kwa madeni makubwa ambazo wanazidai mamlaka za maji, pamoja na uharibifu mkubwa mazingira kwenye madakio ya maji, na hata kusababisha kuingia gharama kubwa ya matumizi ya madawa katika kutibu maji.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi KASHWASA Dk.Judith Kwezi akizungumza kwenye ziara hiyo ya KUWASA Ihelele.
Meneja biashara John Zengo akitoa taarifa ya KASHWASA kwa niaba ya Mkurugenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi KUWASA Stewart Bulaya akizungumza.
Ziara ikiendelea kwenye chanzo cha maji ya Ziwa Victoria Ihelele.
Upandaji wa kwenye tenki la kuhifadhia maji ya Ziwa Victoria ambayo yapo tayari kwa ajili ya kusambazwa kwenda kwa wateja wa KASHWASA.

Post a Comment

0 Comments