Madiwani CCM wadaiwa kutwangana makonde uchaguzi kura za maoni
Diwani wa Ibadakuli manispaa ya Shinyanga Msabila Malale (kushoto) na Diwani wa Vitimaalumu wa Ibadakula Zuhura Waziri.
DIWANI wa Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga Msabila Malale, na diwani wa Vitimaalumu wa Kata hiyo Zuhura Waziri,wamedaiwa kupigana makonde kwenye zoezi la kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) la kuwachagua wagombea ambao watapeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Tukio hilo limetokea jana kwenye Kata hiyo ya Ibadakuli, wakati zoezi hilo likiendelea la upigaji wa kura za maoni la kuwapata wagombea wa CCM, ambao watawania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba 27 mwaka huu.
Diwani Msabila akielezea tukio lilivyokuwa, amesema wakati wagombea walivyomaliza kujidani, na wajumbe kuanza kupewa karatasi za kupiga kura, ndipo akahoji mbona kwenye mfuko wa kuweka kura zilizopigwa hamjajiridhisha kama kuna usalama,na kueleza kwamba baada mfuko kukung’uta ikaanguka kura moja ambayo imeshapigwa.
Amesema baada ya hapo akamuona tena msimamizi wa pili wa uchaguzi huo, akipigia kura watu ambao hawajui kusoma wala kuandika napo akahoji, na kueleza kwamba ndipo Diwani wa Vitimaalumu Zuhura Waziri, ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo akamwambia asiwafundishe kazi na kisha...........
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO NIPASHE