Header Ads Widget

STENDI UNITED WAZINDUA JEZI MPYA

STENDI UNITED WAZINDUA JEZI MPYA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA.
TIMU ya mpira wa miguu Stendi United ya Shinyanga, imezindua rasmi jezi mpya, ambazo zitatumia katika msimu wa ligi ya championship 2024/2025.

Uzinduzi huo umefanyika leo Oktoba 19,2024 katika uwanja wa nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.

Msemaji wa Timu hiyo ya Stendi United Ramadhani Zoro, amesema jezi hizo mpya zinapatika katika maduka mbalimbali kwa bei ya Sh.25000 na zitatumika katika msimu wa ligi ya Championship 2024/2025.

Kocha Mkuu wa Timu ya Stendi United Meja Abdul Mingange, akizungumza kwenye uzinduzi wa jezi hizo mpya, amewaomba mashabiki wa timu hiyo maarufu chama la wana, kwamba wajitojkeze kwa wingi kuiunga timu hiyo, ili endelee kufanya vizuri katika ligi ya Championship na kuja kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara.
“Mchezo wa mpira wa miguu una hitaji kuungwa mkono, tunawaomba mashabiki wa timu ya stendi united wawe pamoja na timu yao muda wote,”amesema Kocha Mingange.

Aidha, ameongeza kuwa kesho watakuwa na mchezo wao hapa Shinyanga, wakicheza na Timu ya Bigman na kuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani ili wapate point 3, na kwamba watakuwa pia na mechi zingine mbili ya Mbeya Kwanza na Biashara United, na kuhitaji kushinda mechi zote ili wapate point 9 na kuendelea kushika nafasi nzuri kwenye ligi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na usajili wa Timu ya Stendi United Chrispin Kakwaya, amesema jezi hizo mpya zina ubora wa hali ya juu,na kwamba stendi zote nchi nzima timu hiyo ni ya kwao yenye makao yake makuu mkoani Shinyanga, na kuwaomba watu wote za stendi waiunge mkono timu yao.

Captain wa Timu hiyo Babilas Chitembe, amesesema wapo tayari kupambana kwa ajili ya timu hiyo ili kuipandisha kushiriki kucheza msimu wa ligi kuu tena,na kuwaomba mashabiki wawaunge mkono.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kocha Mkuu wa Timu ya Stendi United Meja Abdul Mingange akizungumza wakati wa uzinduzi wa jezi mpya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na usajili wa Timu ya Stendi United Chrispin Kakwaya,akizungumza wakati wa uzinduzi wa jezi hizo mpya.
Msemaji wa Timu hiyo ya Stendi United Ramadhani Zoro, akizungumza kwenye uzinduzi wa jezi hizo mpya.
Captain wa Timu ya Stendi United Babilas Chitembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa jezi hizo mpya.
Wachezaji wa Timu ya Stendi United wakipiga picha huku wakiwa wameva jezi mpya.
Wachezaji wa Timu ya Stendi United wakipiga picha huku wakiwa wameva jezi mpya.

Timu ya stendi united ina dhaminiwa na Kampuni ya Jambo.

Post a Comment

0 Comments