Header Ads Widget

NCHIMBI AMPIGIA SIMU NAIBU WAZIRI MKUU DK. DOTTO BITEKO,MAOMBI KAHAMA KUWA MKOA WA KI-TANESCO


NCHIMBI AMPIGIA SIMU NAIBU WAZIRI MKUU DK.DOTTO BITEKO,MAOMBI KAHAMA KUWA MKOA WA KI-TANESCO

katakata umeme wabunge wakosa imani na Meneja wa TANESCO

Na Marco Maduhu,KAHAMA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amempigia simu Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati juu ya maombi ya Wabunge watatu wa Kahama,kwamba Kahama uwe mkoa wa KI-TANESCO ili kuondokana na tatizo la kukatika umeme mara kwa mara.
Dk. Nchimbi amepiga simu hiyo leo Oktoba 10,2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kahama kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Majengo.

Amesema moja ya lengo la ziara yake ni kusikiliza pia kero za wananchi, na kwamba wakati akizungumza na Wabunge wa Kahama kwenye mkutano wa ndani, walimwambia kero yao kubwa ni kukatika kwa umeme mara kwa mara na hivyo kutokuwa na imani na Meneja wa TANESCO, na kuomba Kahama uwe Mkoa wa KI-TANESCO ili kumaliza tatizo hilo.
“Wabunge wenu watatu wa Kahama ambao ni Iddi, Cherehani, na Kishimba wakati na zungumza nao wameniambia kero yao kubwa ni kukatika katika kwa umeme hapa Kahama, na hivyo wanaomba Kahama iwe Mkoa wa KI-TANESCO,”amesema Dk.Nchimbi

“Hivyo ombi hili nalimaliza hapa hapa, nampigia simu Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati alimalize hapa hapa, ombi ambalo hata mimi Katibu Mkuu naliunga mkono,”ameongeza.
Naibu Waziri Mkuu Dk.Dotto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati alipopigiwa simu,amesema awali wameshapata maombi ya wabunge hao wa Kahama, kuwa Kahama uwe mkoa wa KI-TANESCO, na kwamba suala hilo walilifanyia uchambuzi mkubwa, na kuahidi kwamba utakuwa Mkoa wa KI-TANESCO.

Amesema Kahama pia kutajengwa kiwanda kikubwa cha uchenjuaji madini na hata madini ya Kambanga yatachenjuliwa hapo na kuna Mgodi Mkubwa wa dhahabu Bulyanhuru,kilimo cha Tumbaku, kuna Migodi midogo mingi ya madini, hivyo ni lazima kuwepo na umeme wa uhakika.
“Mwaka huu wa fedha 2024/2025 tutakamilisha uchambuzi na tutaupatia Kahama kuwa Mkoa wa Ki-TANESO hivyo wananchi kaeni mkoa wa kula tatizo la kukatika katika kwa umeme lina kwenda kuisha, Dk.Samia anawapenda sana na Kahama mnaipatia mapato mengi Serikali, lazima mpate umeme wa uhakika.”amesema Dk. Biteko.

Aidha, kero zingine ambazo ziliwasilishwa kwa Katibu Mkuu kupitia wasaidizi wake ni 48 zilizowasilishwa na wananchi 33, ambazo amepewa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha azitatue na kumpatia majibu.

Ziara ya Katibu Mkuu Dk. Nchimbi mkoani Shinyanga kesho atahitimisha katika Manispaa ya Shinyanga.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi wa Kahama wkenye mkutano wa hadhara na kumpigia simu Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko juu ya ombi la wabunge wa Kahama,uwe Mkoa wa KI-TANESCO.
Mbunge wa Msalala Iddi Kassim akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Kahama Mjini Jumanne Kishimba akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye mkutano huo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk,Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye mkutano wa hadhara ili kuzungumza na wananchi wa Kahama.

Post a Comment

0 Comments