Header Ads Widget

KIJIRI WA SIMBA AIPA USHINDI YANGA AKIJIFUNGA



KLABU ya Yanga imeibuka mshindi baada ya Beki wa Simba Kelvini Kijiri kujifunga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza Simba ilipata nafasi ya wazi kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Leonel Ateba lakini mlinda lango machachari wa Yanga Djidji Diara kuokoa hatari hiyo na kuwafanya kuwa salama kwenye dakika hizo.


Mpaka kipindi cha kwanza kuisha mechi ilikuwa 0-0, licha ya nafasi nyingi kutengenezwa na nyota wa timu hizo mbili.


Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kwa dakika kadhaa za mchezo ambapo faida ya mabadiliko ilionekana kwa Yanga kwani ilimuingiza kiungo wao mshambuliaji Chama ambaye alitengeneza shambulio la hatari ambalo lilizaa bao kupitia kwa beki wa Simba Kijiri kujifunga akijaribu kuokoa.

Post a Comment

0 Comments