Header Ads Widget

NCHIMBI ANG’OA VIGOGO WA CHADEMA,WAHAMIA CCM

NCHIMBI ANG’OA VIGOGO WA CHADEMA,WAHAMIA CCM

Na Marco Maduhu,KAHAMA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi,amewapokea wanachama 7 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kahama, wakiwamo na viongozi wao ambao wameamua kujiunga na CCM.
Amewapokea wanachama hao leo Oktoba 10,2024 kwenye mkutano wa hadhara wilayani Kahama, ambao umefanyika katika viwanja vya majengo.

Dk. Nchimbi akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao wa CHADEMA 7 na viongozi wao, amesema CCM ina thamini watu wote, na kwamba Katiba yao ina sisitiza binadamu wote ni sawa, na kwamba watu hao wanakaribishwa ndani ya CCM kwa mapenzi makubwa na watapewa ushirikiano.
“Karibuni ndani ya CCM tuna wapokea kwa mapenzi makubwa sana na mtapata ushirikiano, pia taratibu zingine zitaandaliwa za kupewa kadi za CCM.”amesema Dk. Nchimbi.

Aidha, amesema CCM inatambua wajibu wake wa kulea vyama pinzani, pamoja na kuwafundisha siasa safi, na ndiyo chama pekee ambacho kina sera na mipango mizuri, ambayo hutekelezeka na kuwaletea maendeleo wananchi.

Amesema chama hicho pia kimekuwa kikiongozwa na viongozi wazuri wenye sifa zote na wamekuwa wakiwaletea maendeleo wananchi na hata kudumisha amani ya nchi.
Katibu wa Itikadi,Uenezi, siasa na Mafunzo CCM Taifa Amos Makalla, amesema hotuba ambazo amekuwa wakizitoa Mchungaji Peter Msigwa juu ya mabaya ya CHADEMA, zimekuwa zikiwafubua macho wapinzani, na kisha kuhamia CCM kwenye chama ambacho kipo kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

Amesema walipokuwa mkoani Simiyu walipokea pia wanachama wengine wa Chadema, na sasa wamepokea Kahama, na kutoa wito kwa wapinzani ambao wanataka kuhamia CCM waendelee kujitokeza, na kwamba watawapokea na kuwapa ushirikiano wa kutosha.
Aidha, amewataka pia wananchi kwamba kesho wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi, na kisha Novemba 27 wajitokeze kwa wingi kupiga kura, na kuwachagua wagombea wa CCM ambao ndiyo wenye kuwaletea maendeleo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlowa, amewawasihi wana Shinyanga, kwamba zawadi kubwa ambayo watampatia Rais Samia kutokana na kutoa fedha nyingi na kutekelezwa miradi ya maendeleo, ni kumpatia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, na uchaguzi mkuu mwakani 2025.
Naye Mchungaji Peter Msigwa akizungumza kwenye mkutano huo, amewaambia wananchi kwamba Chama ambacho kina jali maslahi ya wananchi ni CCM pekee, vingine vipo kwa ajili ya mashali ya watu wachache, na ndiyo maana viongozi wake wana Ng’ang’ania madaraka ili kujaza matumbo yao.

Mmoja wa viongozi wa Chadema aliyehamia CCM Minja Minja ambaye alikuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Kagongwa, amesema ameamua kuhamia CCM, kutokana na kuona maendeleo makubwa ambayo yanaletwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuridhishwa na utendaji wake kazi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi akipokea wanachama wa CHADEMA 7 ambao wameamua kujiunga na CCM.
Wanachama wa CHADEMA wakikabidhi kadi zao kwa Katibu Mkuu wa CCM.Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi.
Wana CHADEMA ambao wamejiunga na CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi akiwavalisha kofia za CCM Makada wa CHADEMA ambao wamejiunga na CCM
Katibu wa Itikadi siasa,uenezi na mafunzo CCM Taifa Amos Makala akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Rabia Abdalla akizungumza kwenye mkutano huo.
Mchungaji Peter Msigwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye mkutano wa hadhara

Post a Comment

0 Comments