Kamanda wa kikosi cha
Usalama barabarani Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi ameongoza Askari
wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Shinyanga kufanya ukaguzi wa Kushtukiza wa
Mabasi ya abiria yanayofanya safari nyakati za usiku kutoa katika Mikoa ya
kanda ya Ziwa kuelekea mikoa mingine ukaguzi ulioenda sambamba na kukagua
magari madogo sambamba na malori ya mizigo.👇
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi huo ulioanzia katika Stendi kuu ya Mabasi ya Mjini Shinyanga
na kisha kuhamia katika eneo la njia panda ya Tinde – kahama DCP. Ramadjhan Ng’anzi
amesema ukaguzi huo wa kushtukiza unafanyika nchi nzima kwa lengo la kupunguza
ajali za barabarani ambazo zimekuwa zinagharimu Maisha ya watu na mali zao.
Aidha kamanda
Ramadhan Ng’azni amewaonya madereva ambao bado wanakaidi kutii sheria
bila shuruti na kuwataka abiria kupaza sauti wanapoona dereva anaendesha kwa
mwendo hatarishi au kuona gari wanalosafiria linakiuka sheria za usalama
barabarani.
Aidha DCP Ramadhan Ng’anzi amewataka maderva kuwa makini sana katika kipindi hiki kuelekea mwisho wa mwaka na kuwataka kuzingatia sheria za barabarani na kufanya udereva wa kujihami kutokana na ongezeko la watumiaji wa vyombo vya moto unaoenda
sambamba na ongezeko la shughuli za kubinadamu zinazosababishwa na maandalizi
ya sikukuu za mwisho wa mwaka.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464