Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo akizungumza na wazee wa kata ya Maganzo
Suzy Butondo, Shinyangapress Blog
Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo amemuagiza mtendaji wa kata ya Maganzo Stephen Yalomba kuhakikisha wazee wote wenye umri kuanzia miaka 60 anawasaidia ili waweze kupatiwa kadi za msamaha wa kupatiwa huduma za hospitali pindi wanapohitaji huduma hizo.
Licha ya kupatiwa kadi hizo Butondo aliwakabidhi wazee shilingi milioni 1.kwa ajili ya kuanzisha miradi yao, ambapo pia aliiomba kampuni ya mgodi wa almas Williamson Diamond kuwachangia wazee wa maganzo ili wafanye miradi yao waliyodhamilia kuifanya, ambapo pia alikabidhi cheti kwa wazee.
Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na wazee wa kata ya Maganzo katika wilaya ya Kishapu, wakati akizungumza na wazee na kusikiliza kero mbalimbali walizonazo na kuzitatua.
Butondo amesema wazee wengi wamekuwa wakiugua na wanapoenda hospitali wanakosa msaada kwa kupungukiwa fedha, lakini wakisaidiwa na kuwa na kadi za msamaha na wapewe kipaumbele cha kuhudumiwa pindi wanapofika hospitalini.
"Nikuombe afisa mtendaji kwa kushirikiana na mheshimiwa diwani,msimamie hii sera hawa wazee wathaminiwe wapewe hizo kadi na hili zoezi lifanyike kwa kila kijiji ili wazee waandikiwe barua wapewe maelekezo, ili waweze kupatiwa kadi na wapatiwe huduma kwa wakati, serikali ya mama yetu mama Samia Suluhu inawathamini wazee ,"amesema Butondo.
"Wazee wasio na uwezo wa kugharamia huduma za Afya wanatakiwa kupatiwa huduma hizo kwa utaratibu wa msamaha, hata hivyo ni kweli kuna changamoto kwenye baadhi ya maeneo kama hapa wazee bado hawajapata msaada kama kwenye risala yao ilivyosomwa,"amesema Butondo.
"Niwaombe ndugu zangu wa mgodi wa Williamson Diamond muwachangie wazee hawa ili waweze kufanya shughuli zao na kujiongezea kipato, naamini viongozi wetu wa mgodi watafanya hivyo ili kuhakiksha wazee wetu wanajikwamua kiuchumi"ameongeza Butondo.
Butondo amesema wazee kazi yao ni kukemea mmomonyoko wa maadili ubakaji urawiti, na ukatili wa aina mbalimbali katika jamii hivyo ni vizuri kuwaheshimu na kuhakikisha wanathaminiwa na kupatiwa matibabu kwa wakati wanapofika hospitalini.
Akisoma risala katibu wa baraza la wazee kata ya Maganzo John Paul amesema wazee wanauwezo wa kufanya biashara mbalimbali ili waweze kujiongezea kipato wamemuomba mbunge alifiikishe bungeni ili na wao serikali iwakumbuke wapatiwe mikopo, pia wameomba wapatiwe fedha kwa ajili ya kufanya biasharra.
Aidha kiongozi kutoka chama cha wazee wanaume mkoa wa Shinyanga Joseph Masunzu Kuzenza ameiomba serikali kuwapatia wanaume mkopo ili kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kama makundi mengine yanavyopatiwa mikopo.
Baadhi ya wazee Njile Maige na Amina Athuman wamemshukuru mbunge kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata na wilaya kwa ujumla, kwani amefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan, hivyo ni vizuri wakaunga mkono juhudi za mbunge na Rais.

Aidha mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo alizungumza na wananchi wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika maeneo ya soko na kueleza juhudi kubwa za maendeleo zinazoendelea kufanywa na Rais Samia, ambapo amesema serikali kwa awamu ya nne imetekeleza miradi mbalimbali za elimu,afya, maji,barabara,umeme, ambpo katika sekta hizo changamoto zimepungua.
Hata hivyo wananchi wa Maganzo akiwemo Joseph Nkuba amesema wamefurahi kwa kupata taarifa za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na mbunge ndani ya miska minne, hivyo wataendelea kumuunga mkono ili kuhakikisha mahitaji yote yanayohitajika katika kata ya Maganzo yanatekelezwa.
Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Maganzo

Diwani wa kata ya Maganzo Mbalu Kidiga akizungumza kwenye mkutano wa mbunge
Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo akipokelewa na wananchi wa kata ya Maganzo
Wananchi wa kata ya Maganzo baada ya kumpoke mbunge wa jimbo la Kishapu
Wananchi wa kata ya Maganzo wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kishapu

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akipongezwa na wazee wa Maganzo kwa kazi nzuri akizotekeleza na anazoendelea kuzifanya

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace akipongezwa na mchungaji
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa ameshikilia fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kukabidhi kwa wazee wa Maganzo
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akikabidhi fedha shilingi milioni 1. kwa mwenyekiti wa kata ya Maganzo kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali waliyodhamilia kufanya wazee hao
Katibu muenezi wa CCM wilaya ya Kishapu Jiyenze akizungumza kwenye kikso cha mbunge
Mwenyekiti wa kata ya Maganzo akipongeza juhudi za serikali za kuendelea kujenga shule, ambapo ameshukuru kwa kujengwa shule hiyo, ambayo imesaidia kuepusha ajali mbalimbali zilizokuwa zikitokea wakati watoto wakivuka barabara
Mbunge wa jimbo la Kishapu akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutembelea kiwanja ambacho kitatumika kujenga shule ya sekondari kata ya Maganzo
Kiongozi kutoka chama cha wazee wanaume mkoa wa Shinyanga Joseph Masunzu Kuzenza akizungumza kwenye mkutano wa mbunge
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukagua jengo la watoto wenye uhitaji maalumu lililojengwa na serikali
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akikagua jengo la watoto wenye uhitaji maalumu lililojengwa na serikali
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukagua shule iliyojengwa na serikali ili kupunguza adha ya watoto kubanana kwenye shule moja
Mbunge na timu ya viongozi kata ya Maganzo baada ya kukagua jengo la stendi lililojengwa na mfuko wa CSR mgodi wa Mwadui