Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Boniphace Butondo akizungumza kwenye kikao cha Bunge leo Oktoba 31/2024
Suzy Butondo, Dodoma
Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo ameunguruma tena bungeni kuuliza swali juu ya barabara inayotoka kolandoto kwenda Kishapu, yenye kilomita 63 ambayo serikali ilitoa ahadi kuwa itaanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara yenye kiwango cha lami kwa kuanza na kilomita 20 katika mwaka huu wa fedha 2024/2025.
Swali hilo ameuliza leo Oktoba 31 wakati akiwa kwenye kikao cha bunge, kwamba serikali iliahidi katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 itaanza kujenga barabara ya Kolandoto kwenda Kishapu yenye kilomita 63 katika kiwango cha lami na kati ya hizo kilomita 20 zinaenda kuanza katika ujenzi wake, hivyo ni lini serikali itaanza utekelezaji huu.
Jibu hilo lilijibiwa na Naibu waziri wa ujenzi mhandisi Godfley Kasekenya, kwamba Kweli serikali iliahidi kuanza kujenga kwa awamu na kibali tayari kimeshatolewa kwa hiyo taratibu zitakazofuata ni kuanza kuandaa makablasha ya dhabuni ya ujenzi kufuatia ahadi iliyotolewa na serikali
"Kweli serikali tuliahidi kuanza kujenga kwa awamu na kibali kimeshatolewa kwa hiyo taratibu zitakazofuata ni kuanza kuandaa makablasha ya dhabuni ya unenzi kufuatia ahadi tuliyoitoa kwenye kitabu chetu cha bajeti"amesema Naibu Waziri Kasekenya