Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akimkabidhi jiko la gesi mmoja wa mama ntilie wa kata ya Mondo wilayani Kishapu
Suzy Butondo, Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo amegawa majiko ya gesi 20 yenye thamani ya shilingi milioni 1.kwa mama ntilie wa kata ya Mondo kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kutunza Mazingira na kupunguza ukataji wa miti ovyo.
Licha ya kugawa majiko hayo pia amegawa mipira na jezi kwa timu tatu za kata ya Mondo na kutoa mipira miwili katika shule ya msingi Buganika katika kata hiyo, ambapo aliwasihi wanafunzi hao kuendelea na michezo huku wakijisomea kwa bidii ili kuhakikisha wanafaulu vizuri katika masomo yao, ikiwa ni pamoja na kuitunza miundo mbinu ya madarasa inayoendelea kutekelezwa na serikali pamoja na wadau.
Akigawa majiko hayo kwa mama ntilie wakati akiwa kwenye ziara ya kusikiliza changamoto za wananchi ili ziweze kutatuliwa, kueleza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya maiaka minne pamoja na kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, amesema kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha ifikapo 2033 asilimia 80 ya watanzania wote wawe wanatumia nishati safi na salama ya kupikia.
Butondo amesema pamoja na kwamba alitoa majiko ya gesi 200 kwa wananchi mbalimbali wa wilaya ya Kishapu lakini ameendelea kutoa majiko katika mikutano yake kama sehemu ya kuhamasisha jamii kutumia nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya nishati ya miti, ambayo imekuwa ikichangia uharibifu mkubwa wa mazingira katika wilaya ya Kishapu.
"Majiko haya nimetoa kama msaada ili kusapoti jitihada za Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha malengo ya serikali ya kutunza mazingira yanatimia, na kuhakikisha jamii inaishi mahali salama lakini pia vizazi vjavyo kwa ujumla viweze kukuta mazingira safi,"amesema Butondo.
"Pia Serikali imesema itaendelea kuhamasisha wananchi kujua umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuhakikisha utunzaji wa mazingira nchini unaendelea kwa kugawa mitungi ya gesi katika makundi mbalimbali ya wajasiriamali na mama ntilie katika maeneo mbalimbali, kuendana na kuendana na mabadiliko ya tabia nchi " ameongeza Butondo
Aidha wananchi wa kata hiyo walitoa kilio chao mbele ya mbunge kwamba kata hiyo haina maji safi na salama kwani maji wanayotumia si salama yamekuwa yakisababisha wananchi kupata magonjwa ya kuhara ikiwa ni pamoja na ndoa nyingi kuachika kutokana na mwanamke kwenda kutafuta maji umbali wa kilomita zaidi ya kumi ambayo mia si salama.
"Mheshimiwa mbunge tunakushukuru sana kwa kuendelea kutekeleza ahadi zao nyingi kwa kushirikiaba na Rais Samia Suluhu na diwani wa kata yetu, lakini bado tunakabiliwa na changamoto ya ukosekanaji wa maji safi na salama, hiki ni kilio kikubwa sana tulichonacho, kwani watoto wanapata ajali mbalimbali za kugongwa na gari au pikipiki wengine kubakwa na ndoa zetu kutokuwa na amani kutokana na ukosekanaji wa maji,"ameeleza Pendo Michael
"Tunakuomba sana mbunge wetu utufikishie ujumbe huu kwa Rais wetu mama Samia atuhurumie atuletee mradi wa maji tunapata shida sana, kweli tunaona inatekeleza lakini tunaomba sana na suala hili la maji litekelezwe kwa wakati ili tuweze kunusuru ndoa zetu na kuondokana na ajari zisizo za lazima"amesema Willliam Ndondi
" Maji tunayotumia katika kijiji cha kabila ni maji machafu sana ya kutoka chini na sasa imeibuka hali ya kuharisha na kutapika inawezekana ni kutokana na maji hayo ambayo ukiyaona mheshimiwa yanafanana na maziwa hata ukioshea vyombo havitakati tunaomba serikali yetu itukumbuke na sisi hali ni mbaya"Jonathan Bundala
Kwa upande wake diwani wa kata ya Mondo William Jijimya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu, amesema kweli kata hii inachangamoto kubwa ya maji, hivyo alimuomba mbunge alibeba ili kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa wakati,ili wananchi waendelee kuwa na amani, aidha diwani alimpongeza mbunge kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika wilaya ya Kishapu.
Baada ya maswali ya wananchi Mbunge wa jimbo la Kishapu Butondo alitoa maelekezo kwa meneja wa Ruwasa Dickson Kamazima amesema kweli wilaya ya Kishapu kame lakini tayari wameshafanya usanifu hivyo wanaendelea kutafuta fedha ili waendelee kutekeleza miradi ya maji ili wananchi wasiendelee kupata shida ya maji
Aidha Butondo baada ya kumaliza mkutano wake aliteta na mabalozi wote wa kata hiyo nakuwaomba waendelee kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unaanza 27 Novemba mwaka huu.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akimkabidhi jiko la gesi mmoja wa mama ntilie wa kata ya Mondo wilayani Kishapu
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Mondo
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Mondo
Diwani wa kata ya Mondo William Jijimya akizungumza kwenye mkutano wa mbunge uliofanyika kata ya Mondo
Katibu muenezi wa wilaya ya Kishapu Jiyenze Seleli akizungumza kwenye mkutano wa mbunge uliofanyika kata ya Mondo
Mwenyekiti wa CCM kata ya Mondo akizungimza kwenye mkutano wa mbunge
Katibu wa CCM kata ya Mondo Donald Nyerere akizungumza kwenye mkutano wa mbunge
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu Dickson Kamazima akijibu hoja za wananchi kuhusu maji
Wananchi wa kata ya Mondo wilaya ya Kishapu wwkimsikiliza mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo
Wananchi wa kata ya Mondo wilaya ya Kishapu wwkimsikiliza mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiburudika na wananchi wake wa kata ya Mondo wakati wakimpokea
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiburudika na wananchi wake wa kata ya Mondo wakati wakimpokea
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiburudika na wananchi wake wa kata ya Mondo wakati wakimpokea
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiburudika na wananchi wake wa kata ya Mondo wakati wakimpokea
Mbunge wa jimbo la Kishapu Butondo akisaini kitabu katika ofisi ya mwalimu mkuu shule ya msingi Buganika kata ya Mondo
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Buganika ambapo amewataka watunze miundo mbinu ya madarasa
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Buganika ambapo amewataka watunze miundo mbinu ya madarasa
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akikagua jengo la shule ya msingi Buganika lililojengwa kwa fedha ya CSR kutoka kampuni ya mgodi wa Williamson Diamond
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akikagua jengo la shule ya msingi Buganika lililojengwa kwa fedha ya CSR kutoka kampuni ya mgodi wa Williamson Diamond