Familia ya Petro Sayi ikiwa kwenye picha ya pamoja
Suzy Butondo, Shinyanga
Mkazi wa kijiji cha Bugomba B Kitongoji cha Shilabela kata ya Ubagwe Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Petro Sayi amejikuta akilia baada ya kudaiwa Ng’ombe sita zilizotolewa kwaajili ya Mahari ya kuolewa binti yake nakurudishwa nyumbani kwa kudaiwa hazai.
Akizungumzia mkasa huo baba huyo wa familia Sayi ameeleza mkasa huo mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye kijiji hicho,na baadhi ya wazee na majirani walioshuhudia utolewaji wa ng"ombe hizo tangu mwaka 2017 alipokuwa akiolewa binti yake.
Sayi amesema binti yake aliolewa na kuishi na mume wake katika kata ya Nyankende kwa muda wa miaka minne, ambapo alishangaa mwaka jana binti yake kudangaywa na mume wake kuwa wazazi wako wanakuhitaji ndipo alipomleta akiwa alivyo vaa bila mzigo wowote nakumfikisha nyumbani kumkabidhi nakueleza ameamua kumleta kwao kwa sababu hazai tangu amemuoa.
“Siku hiyo nilikua nikiendelea kufanya kazi hapa nyumba bila kuja hili wala lile nilishtukia nikaona pikipiki inakuja nyumbani kwangu nikapsema nimepata wageni kumbe ameletwa mwanangu kaachika kwa kosa la kutozaa"alieleza Sayi.
"Niliwapokea huku nikiwa na furaha kuwa wamekuja na mme wake kutusalimia, walinisalimia na mkwilima wangu alinsalimiabaada ya salamu akaniambia kuwa amemrudisha binti yangu kwa sababu hazai nilinyamaza kimya baadae nikamshukuru na kumwambia nashukuru kwa kuwa umemrudisha akiwa mzima aliondoka mme wake nikabaki na mwanangu"aliendelea kueleza Sayi.
"Baada ya mwaka mmoja nililetewa taarifa ya kuitwa Mahakama ya Mwanzo Mpunze nakutolewa hukumu kuwa nirudishe Ng’ombe saba sababu mwanangu ametia hasara alikoolewa hazai ndipo nikajiuliza kumbe nirudishe kama nilikopeshwa sio zawadi yangu kama mzazi"alisema Sayi.
AKIELEZA MKASA ULIOMPATA BINTI
Binti aliyeolewa Anastazia Sayi (21) alisema aliolewa tangu mwaka 2017 baada ya kuolewa alifikia ukweni kwa mama mkwe, ambapo alikuwa akifanya kazi mbalimbali zikiwemo za kilimo na kuchunga mifugo.
"Nilikaa mwaka mmoja kwa mama mkwe baadae tukajitegemea mimi na mme wangu, tukatoka hapo kwa mama mkwe,lakini mama mkwe aliendelea kunifuatilia kwa kunitukana kwamba mimi mwanamke gani sizai hivyo alikuwa akimtaka mtoto wake aniache aowe mke mwingine"ameeleza Annastazia
"Kwa kweli niliteseka sana mimi nilteseka kwa kuchunga mifugo ya ukweni na kupika, mama mkwe wangu alikuwa akinitesa na kunilazimisha nifanye kazi zote kwa sababu sina faida zozote, na alikuwa akimlazimisha mtoto wake asinipende atafute mwanamke mwingine ili mimi anirudishe nyumbani kwetu kwa sababu sizai na wazazi wangu warudishe ng’ombe walizotoa"ameendelea kueleza.
“Nikiwa kwangu na mme wangu mama mkwe alimuita mume wangu akamueleza kwamba turudi kuishi naye, mme wangu alikubali tukarudi nyumbani tena na ndipo mateso yakaendelea na hapo mme wangu alimshawishi aniache aoe mke mwingine ndipo alipata mwanamke mwingine senta yaani madukani alianza kulala huko na kuniacha mimi nyumbani nikilala peke yangu"ameeleza.
" Niliendelea kuvumilia hivyo hivyo huku mama mkwe akimwambia mme wangu kuwa asiwe anaenda kwa mwanamke huyo bila kula awe anakula kwanza ndo aende, baadae aliowa mwanamke mwenye watoto watatu ambao siyo watoto wake niliendelea kuvumilia hivyo hivyo, walipoona sishituki ndipo mme wangu alikuja na pikipiki akaniambia twende nyumbani kwenu tukawasalimie nilipanda kwenye pikipiki hivyo hivyo nilivyokuwa nimevaa,"
Tulipofika nyumbani nikashangaa nakabidhiwa kwa baba nikamuuliza mme wangu kuwa imekuwaje tena uliniambia tunakuja kusalimia tu na kurudi hakunijibu akaondoka na mpaka sasa nipo, mme wangu alikuwa ananipenda na mimi nampenda ila mama mkwe ndio alikuwa hanipendi ananiambia mimi mugumba sizaagi sifai kuendelea kukaa hapo ” alisema Sayi.
Kwa upande wake shuhuda ambaye ni jirani wa familia hiyo Faustine Kayanda amesema baada ya miaka mitatu waliitwa kama wazee kupata taarifa kuwa binti karudishwa nyumbani sababu hazai na kitu kilichowashangaza mzazi kuombwa arudishe ng’ombe mila na desturi za kabila la wasukuma Mahari ni zawadi.
"Kwa kweli na sisi limetushangaza sana hili binti wamekaanae miaka mnne akiwafanyia kazi mbalimbali halafu wanamrudisha na kuanza kudai mahali zao tena hadi kufikishana mahakamani sisi tunajua ukipewa mahali ni kama zawadi tu lakini mama mkwe wa huyu binti anataka Ng"ombe saba arudishiwe "ameeleza Kayanda
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho Msafiri Hussein alisema kweli familia hiyo ilifika ofisini kupata ushauri wakati akiwa mwenyekiti baada ya binti kurudishwa nyumbani na ng’ombe ziliamriwa kurudishwa ila walishauriwa familia ya Sayi irudishe ng’ombe wawili au shilingi laki mbili, lakini hawakuafikiana walishangaa kesi ikaenda mahakamani nakutolewa hukumu ng’ombe zote zirudishwe.
“Nitoe ushauri wangu kwamba jamii ipewe elimu mahari iwe kama zawadi iandikishwe ili badaye isiwe mateso kwa mzazi sababu unapopewa ng’ombe hizo na baadaye kudaiwa hufikirii binti katumikishwa usiku na mchanga naye kapata hasara hakuna wa kumuoa tena”alisema Hussein.
Mama mkwe wa binti huyo Lusia Lushinge alisema kweli amemrudisha binti huyo na kudai ng’ombe ambazo alimpa mwanaye atoe Mahari sababu binti hakukaa nyumbani kwake muda mrefu alikuwa akirudi nyumbani kwao bila faida yoyote na kijana wake hayupo amesafiri kwenda mkoani Katavi.
Baba mzazi wa Annastazia Sayi akizungumzia tukio hilo
Annastazia Sayi ambaye alirudishwa nyumbani kwa kosa la kutopata mtoto akizungumzia tukio hilo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Bugomba B Msafiri Hussein akizungumza
Mmoja wa mashuhuda waliosikitishwa na kudaiwa kwa mahali hiyo
Mmoja wa mashuhuda waliosikitishwa na kudaiwa kwa mahali hiyo
Mama wa binti Annastazia akieleza kusikitishwa kwa kudaiwa kwa mahali ya mtoto wake
Mmoja wa mashuhuda waliosikitishwa na kudaiwa kwa mahali hiyo
Mmoja wa mashuhuda waliosikitishwa na kudaiwa kwa mahali hiyo