Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Shinyanga
imewataka viongozi wa dini kuwahamasisha waamini wao kujiandikisha na kupiga
kura sambamba na kuchukua tahadhari juu ya vitendo vya rushwa vinavyoweza
kujitokeza katika mchakato mzima wa maandalizi ya uchaguzi huo huku baadhi ya wazee
maarufu wa Mkoa uo wakidai kuwa zoezi la kujiandikisha linaenda kwa kusuasua
hali ambayo inaweza kuathiri uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 mwezi wa 11 mwaka huu.
Na Mwandishi wetu kutoka Nkoani Shinyanga.
Hata hivyo Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
mkoa wa shinyanga Bw. Donasian Kessy ametoa wito kwa viongozi wa Dini
ambao wamehudhuria semina iliyoandaliwa na TAKUKURU na kufanyika katika ukumbi
wa taasisi hiyo kuisaidia serikali kuwaomba waumini wao kushiriki mchakato
mzima wa zoezi la uchaguzi kwakua wao ndio wenye dhamana ya kuchagua viongozi
wanaowataka.
Mchungaji Yohana Ernest Nzelu ni Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ametoa wito kwa waumini wa Kanisa la KKT Pamoja na wananchi wote kutopuuzia zoezi la kujiandikisha na kupiga kura kwakuwa ndiyo fursa pekee ya kuchangua viongozi watakaosaidiana na Serikali kusimamia miradi ya maendeleo kwa ajili ya maendeleo ya jamii yote ya Taifa la Tanzania.
Hata hivyo Pamoja na jukumu la TAKUKURU la kuzuia na kupambana na rushwa imeshauria kuchunguza kwa undani zaidi mambo yanayofanywa na viongozi baadahi wenye nafasi kubwa serikalini yanayoashiria rushwa kwakuwa yanaweza kuutia dosari uchaguzi huo.
Pamoja na hayo viongizi wa Dini wameitaka Serikali kujenga ofisi
za TAKUKURU kwenye ngazi za chini vijijini ngazi ya kata na vijiji kwakuwa huko
pia vitendo vya Rushwa vinafanyika hususani rushwa ya Ngono.
Hata hivyo Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU imewakumbusha Wananchi kauli mbiu ya Taasisi hiyo inayosema kuwa “Jukumu la kupambana na rushwa ni lako na langu,sote kwa Pamoja tushiriki kupambana nayo na kuitokomeza
Viongozi wa dini wilaya ya Shinyanga wakifatilia mada za rushwa katika uchaguzi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464