UTALII WA NDEGE NA WANYAMA KATIKATI YA MAJANGA YA KIMAZINGIRA

 UTALII WA NDEGE NA WANYAMA KATIKATI YA MAJANGA YA KIMAZINGIRA



 Hili ndilo tukio la kusisimua zaidi analotarajia mtalii wa  maisha ya  ndege pori,kuamshwa alfajili na sauti mseto za  mashindano ya nyimbo zinazotokea juu ya miti.

 Sauti hizo humpa mtalii hakikisho la moja  kwa moja  kwamba katika safari yake atapata picha za kutosha za ndege.Sauti zinatoa ishara ya kuwepo uhai wa mazingira  na viumbe vyake.

Sio kila nchi duniani inaweza kuwa na matukio ya aina hii isipokuwa katika hifadhi zetu ,zenye mifumo asili ya kiikolojia inayoratibu uhusiano mwema wa viumbe na mazingira yao.

 Safari za kupokea wageni wanaofika kufanya utalii wa ndege haziwezi kukoma leo, kwa sababu ndege wengi wa porini hawafugiki,ni lazima uwakute kwenye mazingira yao ya asili.

Hata hivyo kuna tishio kubwa  linalowakabili ndege hao kwa sasa,kutokana na uharibifu wa mazingira.Hiki ni kilio cha binadamu,ndege na wanyama.Mimea inapukutisha majani  kwa wingi Ili kubana matumizi ya maji sababu ya ukame.

Tishio hili linaanzia vijijini ambapo zamani,ndege kama  kware na kanga walifika hadi kwenye kiambaza cha nyumba,Mazingira yalikuwa raffiki i,upande wa pili kuna uhasama wa binadamu na wanyama.

Hali hii tayari imewashtua wataalamu wa maisha na tabia za ndege,ambapo Dkt Jason John kutoka Idara ya Zoolojiia na Wanyamapori Chuo Kikuu Dar es Salaam,anasema kuna mifano hai ya. ndege walioanza kupotea kutokana na uharibifu wa mazingira.

 Mtaalam huyo ambaye ni mbobezi katika tafiti za maisha na tabia za ndege,anamtaja korongo nyangumi kuwa yuko hatarini kutoweka,kama jitihada za kulinda maisha yake hazitakuwa maradufu.



 "Maeneo yao mengi ya asili yalivamiwa na mifugo, hupenda kujenga  kiota mfano wa mtumbwi ardhini, mayai yao yanaharibiwa  kuhusu chakula chao hupenda kuwinda samaki kando ya mito na mabwawa"anasema Dkt John

Mtaalam huyo anasema, kuanzishwa kwa  hifadhi za Burigi Chato na Kigosi ni habari njema kwa kuwa ni makazi ya asili ya ndege hao.Mdomo wao mkubwa mfano wa kiiatu huwpa sifa ya ziada.

Aidha ameandika vitabu tofauti kuhusu maisha na tabia za ndege, miongoni mwake ni kitabu kiitwacho"The Birds of Western Tanzania"au ndege wa Magharibi mwa Tanzania, kinatumika kama rejea maeneo mengii duniani.

 Korongo nyangumi anaishi ukanda wa Kagera na Kigoma pekee hapa nchini, chakula chake kikuu ni samaki walnaopatikana kwenye mito na mabwawa vilivyoathiriwa na uharibifu wa mazingira.

 Uzuri wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo haunogi  biila ndege aina ya tandawala(Denhams Bustard)ambaye sifa yake kubwa ni kusafiri mwendo mrefu  angani kutoka bara moja hadi jingine.

 Ndege huyo huvuta wageni kufanya utalii wa kupiga picha katika hifadhi hiyo, ambapo sababu zozote za uharibifu wa mazingira zinaweza kuwakimbiza ndege hao na itakuwa vile vile kwa watalii.

Tayari hifadhi inakabiliwa na changamoto za miti na vichaka vamizi, vinavyoathiri mito  na vijito na inatishia uhai wa mimea ya asili na viumbe hai waliomo.

 Hifadhi ya Taifa Serengeti ni makazi ya maelfu ya ndege.Sehemu ya picha zake zimetengeneza maudhui kwenye Filamu ya "The Royal Tour" ambayo muongoza watalii kinara ni Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan

 Filamu hiyo inawaeleza  wageni kwamba Serengeti ni chaguo bora zaidi la kufanya utalii wa kupiga picha za ndege wa porini.Kuna ndege mnana na jamii zote za tai na korongo.

Maajabu katika filamu ya "The Royal Tour"yanatajwa kote duniani.Katika mtandao wa www.dumasclarion.com wa Marekani,Mwandishi wa Shirika la Associated Press(AP)David Bauder,katika  makala yake anamtaja Rais Samia Suluhu Hassan ,kama muongoza watalii kinara anayeifungua nchi kupitia filamu yake

 Anasema ni kiongozi aliyebeba wajibu wa kuieleza dunia kweli,kuhusu usalama wa wageni watakapofika nchini hasa baada ya janga la virusi vya COVID 19,ambavyo vilidhoofisha sekta ya utalii na mifumo mingine ya dunia.

 Aidha makala hiyo imenukuliwa katika mtandao wa www.nzherald.co.nz wa  New Zealand ,huku wageni wengi wakimiminika nchini baada ya kuvutia na vivutio ndani  filamu hiyo.

 Baadhi ya watalii waliofika nchin mara ya kwanza, baada ya filamu hiyo wanaeleza hisia zao,kupitia mtandao maarufu wa  www.tripadvisor.com.Ni jukwaa  la watalii kutoka Mataifa mbalimbali duniani

 Pia kupitia mtandao huu,maelfu ya watalii hulitumia kupiga kura  kupitisha vivutio bora zaidi duniani,

Tuzo zinazoratibiwa na Taasisi ya World Travel Awards kila mwaka

Tarehe 18,Oktoba 2024 Serengeti ilitangazwa kuwa Hifadhi bora Afrika,ukiwa ni ushindi wa sita mfululizo huku Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikitajwa kuwa kivutio bora zaidi Afrika.

Kupitia mtandao huo,mtalii aliyejitambulisha kwa jina la Rachely kutoka Houston,Texas anasifia uzuri wa Serengeti,huku akitaja  orodha ndefu ya ndege na wanyama na kumsifia muongozaji kwamba alikuwa na maarifa ya kutosha ya kazi yake.

"Hii ni safari ya kukumbukwa maishani,tulianzia Tarangire na kwenda Serengeti hapa tulifurahi kuona wanyama na ndege wengi wa kuvutia muongozaji wetu alikuwa mwema sana,alikuwa na maarifa ya kutosha kwa kila jambo tulilouliza"anaandika Rachely

Pia kupitia mtandao huo wa Trip Advisor Isabellla.A anafurahia maisha ya mitaani Jijini  Arusha na umakini wa muongoza aliyehakilisha wako salama barabara,pamoja na watoto wao wawili wadogo.

Baadhi ya watalii wanaofika nchini, wakati wa utoto walikuja na wazazi wao,baada ya kukua na kujitegemea hupenda kurejea historia ya maisha yao kwa kurejea maeneo waliyofika na wazazi wao.

Tishio la kutoweka kwa ndege, haliwezi kuwaacha salama wanyamapori.Viumbe hivi vinaishi kwa kutegemeana.Tai mzoga au tumbusi hutegemea mabaki ya mawindo.Kwa njia hiyo husafisha hifadhi na kudhibiti uwezekano wa usambaaji wa virusi vya magonjwa.

Kengele ya tahadhari kuhusu athari za uharibifu wa mazingira,pia imelia  kwa mnyama sheshe au puku ambaye kasi ya kutoweka katika maeneo yao ya asili ni kubwa.

 Sensa iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(Tawiri)na matokeo kuchapishwa kwenye tovuti yao mwaka huu 2024,yanatioa  tahadhari katika mifumo ikolojia mitatu ya Nyerere-Selous na Mikumi.

Sensa hiyo ambayo hufanyika kila baada ya miaka mitamo,inasema idadi  yao imeporomoka kutoka  idadi ya 1,579 mwaka 2018 hadi 496 mwaka 2022, maeneo yao ya asili ikitajwa ni mapori ya akiba ya Kiilombero na ziwa Rukwa.

 Pia matokeo ya utafiti wa sensa ya mwaka 2020 katika hifadhi ya Burigi Chati yanataja kuonekana kwa pofu,wanyama ambao hawakuonekana katika sensa ya mwaka 2014,huku pundamilia wakiongezeka kwa asilimia 22.

 Mtafiti kutoka katika Taasisi hiyo Dkt Edward Kohi anasema,hata malalamiko ya wananchi kwamba wanavamiwa na tembo ni matokeo ya uvamizi wa maeneo yao ya  asili ambayo wananchi wameweka makazi na shughuli za kilimo.

 "Ni matokeo ya mabadiliko ya utamaduni wa chakula chao,sio kwamba tembo wameongezeka wananchi wanalma kwenye maeneo yao ya asili,tembo wanaona kuna chakula kipya wanaanza kukifuata anasema Dkt Kohi

 Katika Hifadhi ya Ziwa Manyara watalii hufurahi kupiga picha za maelfu ya ndege aina ya flamingo,ambao muunganiko wao katika ziwa hilo lenye magadi huonekana kama mfano wa shuka kubwa jeupe.

 Muongoza watalii na Mkurugenzi wa Bukoba Tours William Rutha,anasema watalii  hupenda kuona vivutio vingi katika eneo moja,huku wakitaka kupiga picha za kumbukumbu za ndege,,wanyama na vivutio vingine.

 Hapa ndipo kuna kusanyiko kubwa zaidi la ndege wahamao kutoka mabara ya Asia na Ulaya, kuna majukwaa kukuwezesha kupiga  picha kwa karibu na kutazama wanyama kama viboko kutoka mita chache.

Kusanyiko la ndege hao ni vikao vya manung'uniko dhidi ya uharibifu wa mazingira yao ya asili ,wakionya  utiririshaji wa maji yenye kemikali za sumu kutoka viwandani wakati wa kilimo kwenye ziwa Manyara ukomeshwe.

 Mwisho





 Maelezo ya picha

 1.Makundi ya ndege aina ya flamingo katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.Picha kwa hisani ya Hufadh ya Taifa Ziwa Manyara


2.Ndege aina ya Korongo Nyangumi ambaye yuko hatarini kutoweka duniani Picha kutoka mtandao wa Getty images


3.Watalii wakiangalia ndege kutoka jukwaani atika Hifadhi ya Ziwa Manyara.Picha kwa hisani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara


4.Ndege wakiwa kwenye makazi yao katika Kisiwa cha Musira ndani ya Ziwa Victoria,Manispaa ya Bukoba.Picha na Phinias Bashaya

 

5Mkazi wa Kisiwa cha Musira kilichopo Ziwa Victoria Manispaa ya Bukoba Mikoani Kagera  akiharibu viota vya ndege.Picha na Phinias Bashaya

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464