USAJILI WA VITUO VYA KULEA WATOTO DAR MCHANA DAR WAONGEZEKA

 

                                                  Na Patricia Kimelemeta

MKoa wa Dar es Salaam umekuza na mafanikio makubwa katika usajili wa vituo vya kulea watoto mchana (DCC) kutokana na hamasa  inayotoleea na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaotekeleza Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi Malezi na Maendeleo ya Awali ya watoto (PJT-MMMAM).Programu hiyo ilizinduliwa Mwaka 2021 ambao inashirkisha Serikali kuitia wizara mtambuka, Asasi za kiraia na waandishi wa habari na kuhusisha watoto wenye umri kuanzia sifuri hadi miaka minane.

Katika programu hiyo, wadau wnaatekeleza afua tano za elimu, afya, Lishe, Malezi yenye mwitiko na ulinzi na usalama.Akizungumza hivi karibuni, Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar Es Salaam, Nyamara Elisha amesema kuwa, wakati wanaanza kutekeleza Programu hiyo waliweza kusajili vituo 1626 kati ya 4000 ambavyo vilikua vikiendesha shughuli zake bila ya kusajili, lakini mpaka sasa wameweza kusajili vituo zaidi ya 2000 huku zoezi Hilo likiendelea.

"Hayo ni mafanikio makubwa ya utekeleza wa PJT-MMMAM, kwa sababu, miaka  iliyopita wamiliki wa vituo walikua wakiendelea kusajili watoto bila kufuata utaratibu wa kisheria pamoja na kuwafundisha bila ya kusajili kituo, lakini sasa hivi hali ni tofauti, wamiliki wanakuja kusajili vituo vyao na wengine wanaboresha miundombinu ya majengo na vyoo ili viweze kukidhi matakwa ya kisheria," amesema Elisha.

Amesema kuwa vituo vingine vinaendesha shughuli zao bila kusajili jambo ambalo limewafanya kuwataka kuboresha mazingira na kuvisajili ili viweze kutambulika.

Amesema kuwa  vituo hivyo vinachukua watoto kuanzia umri wa miezi sita hadi miaka mitano ambapo baadhi yake havina ubora, ulinzi na usalama wa mtoto ni mdogo jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha wawapo kituoni hapo.

" Kuna baadhi ya vituo ambavyo vimefunguliwa kwenye mazingira duni,  miundombinu yake hairidhishi kwa sababu inaweza kuhatarisha maisha ya mtoto, tulizungumza na wamiliki ili waweze kuboresha mazingira ili watoto wakae mahali salama," amesema.

Amesema kuwa, walezi wa vituo hivyo hawana sifa na wengine wamechukuliwa kutokana na mahusiano yao na wamiliki wa vituo hivyo na kuwalipa mishahara midogo.

" Vituo vingi wafanyakazi wake hawana elimu ya malezi, wamechukuliwa kutokana na uhusiano wao na wamiliki Kwa sababu wanawalipa mishahara midogo hivyo basi hawawezi kuwa makini kama mlezi ambaye amepatiwa elimu ya malezi," amesema.

Ameongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, serikali iliwapa miongozo ya namna ya kuboresha miundombinu hiyo pamoja na kuwataka kutafuta walezi wenye sifa,jambo ambalo limefanikiwa Kwa kiasi kikubwa.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki wa vituo va kulea watoto mchana,Shukuru Mwakasege amesema kuwa tangu Serikali ilipoanza kutekeleza Programu ya PJT-MMMAM wamiliki wa vituo hivyo waliweza kusajili Umoja huo pamoja na kufuata mwongozo iliyotolewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kutafuta walezi wenye sifa.

" Tulipoanza kutekeleza PJT-MMMAM tukaanza usajili vituo n kufuata mwongozo iliyotolewa na Serikali, lakini pia tumeweza kupata mafunzo ya malezi toka kwa wadau mbalimbali ya namna ya kuboresha miundombinu na kupata walezi wenye sifa, ndomana hata usajili wa vituo vya watoto umeongezeka," amesema Mwakasege.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamesema kuwa, ujip wa PJT-MMMAM umesaidia kuongeza uelewa kwa wamiliki wa vituo vya kulea watoto mchana kuboresha miundomnu ya kujifunza kwa watoto pmoa na. wazazi kuwapeleka watoto vituoni hapo kwa ajili ya kujifunza watoto.

" Sasa hivi kidogo kuna mwamko wa uboreshaji wa miundombinu ya kujifunza watoto wetu,tofauti na hapo nyuma ambapo mtu anajenga jiko na kuchukua watoto na kuanza kufundisha," amesema Khamis Jumanne mkazi wa Kigogo.

Mwisho

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464