WALIMU SHYDC WAPIGWA MARUFUKU KULIMA MASHAMBA YA SHULE,KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI

WALIMU SHYDC WAPIGWA MARUFUKU KULIMA MASHAMBA YA SHULE

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WALIMU katika Shule za Msingi na Sekondari wilayani Shinyanga, wamepigwa marufuku kulima kwenye mashamba ya shule,ili mashamba hayo yatumike kwa ajili ya kulimwa chakula cha wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro.

Maagizo hayo yametolewa leo Novemba 5,2024 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro, wakati akitoa salamu za viongozi, kufuatia hoja ambayo iliibuliwa na Diwani wa Nyida Seleman Segeleti, juu ya Walimu kuendelea kulima kwenye mashamba ya shule na wakati walizuiwa.

Mtatiro amesema Walimu hawazuiwi kufanya shughuli za kilimo kama sehemu ya kujiongeza kipato na kupata chakula, lakini suala la kulima kwenye mashamba ya shule hilo hapana, bali wanapaswa kukodi mashamba kwa wanakijiji na kufanya shughuli hizo, ili mashamba hayo yatumike kwa ajili ya kulimwa chakula cha wanafunzi.
Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje.

“Mshamba ya shule yatumike kwa shughuli za shule ili wanafunzi wapate chakula, na siyo Walimu kulima Mashamba hayo,”amesema Mtatiro.

Ameeleza kuwa Walimu kuendelea kulima kwenye mashamba ya shule, ni kuleta Mgogoro kwa jamii ambayo ipo tayari kulima mashamba hayo ili watoto wao wapate chakula shuleni, sababu wengine uwezo wa kuchangia chakula hawana, na kwamba tatizo hilo lilishatokea Manyada ambapo wazazi waligoma kuchagia chakula kutokana na mashamba ya shule kulimwa na Walimu, na wakati wao walikuwa wapo tayari kwenda kuyalima.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje,akizungumzia tatizo hilo,amemuangiza Mkurugenzi kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata, kwamba aandike barua pamoja na kuambatanisha Waraka wa kuzuia Walimu kulima kwenye mashamba ya shule, na wepewe pia Madiwani na kusambazwa kwa shule zote ili kumaliza tatizo hilo.

Mthibiti Mkuu wa ubora wa shule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joyce Andrew, awali akijibu maswali ya Madiwani, amesema kwamba Waraka wa Walimu kuzuiwa kulima kwenye mashamba ya shule walishapewa na kusambazwa kwenye Kata zote.
Diwani wa Nyida Seleman Segeleti, awali akizungumza kwenye baraza hilo, aliibua hoja kwamba kuna taarifa ilitolewa kuwa Walimu wasilime kwenye Mashamba ya shule hasa yale yenye Rutuba, lakini katika shule ya Msingi Nduguti ameshaghaa kuona Walimu wakilima mashamba hayo, tena kwa kutumia Trekta na kuibua malalamiko kwa wananchi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI KIKAO CHA MADIWANI👇
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Madiwani wa Halamshauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464