HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA INA ADHIMISHA WIKI YA KISUKARI KWA UPIMAJI MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA BURE

IKIWA ni wiki ya Kisukari Duniani, Hospitali ya Rufaa Mkoa Shinyanga leo Novemba 12, 2024 imeanza maadhimisho kwa kuendesha zoezi la Upimaji wa Magonjwa yasiyoambukiza bila malipo katika Stendi ya Soko Kuu iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

Zoezi hilo litahusisha upimaji wa magonjwa ya Shinikizo la Juu la Damu, Kisukari pamoja na uzito, lakini vilevile litahusisha utoaji wa elimu kuhusu magonjwa hayo na elimu ya lishe.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga imedhamiria kufanya maadhimisho hayo kwa siku tano (5) hadi Julai 16, 2024, lengo na madhumuni ni kusaidia kujua hali zao za kifya, pamoja na kuokoa maisha yao.

Vilevile, mbali na kushiriki katika maadhimisho, Hospitali imeendelea kufanya jitihada za kuhakikisha inaokoa maisha ya watanzania, kwa kuwahamaisha wateja wake (wagonjwa), kuwa na desturi ya kufika Hospitalini kwa ajili ya kupata vipimo zaidi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Muda ni Sasa, Zuia Maambukizi ya Magonjwa yasiyoambukiza Mahala pa Kazi".
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464