BOT YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA

BoT yawajengea uwezo waandishi wa habari Kanda ya Ziwa,kuondoa mzunguko wa noti za zamani wagusiwa

Na Marco Maduhu,MWANZA

BENKI kuu ya Tazania (BoT)Tawi la Mwanza,imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa,kwa ajili ya kuwajengea uwezo namna ya kuhabarisha umma kuhusu masuala ya benki hiyo kwa usahihi,na kuondoa maswali kwa wananchi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza kutolewa leo Novemba 14 hadi 15, yanafanyika katika ukumbi wa mikutano katika benki hiyo,yakihusisha baadhi ya waandishi wa habari kutoka Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu,Kagera na Mara.

Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania Tawi la Mwanza Gloria Mwaikambo,akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwa waandishi wa habari,katika kuelimisha umma juu ya masuala ya uchumi,fedha na biashara.
Amesema waandishi wa habari wakielewa zaidi masula ya Benki kuu,itasaidia kuelimisha umma kwa kuwapasha habari kwa usahihi,na kwamba kwa sasa kuna uamuzi wa kuondoa mzunguko wa noti za zamani,pamoja na kutambua alama za fedha halali, jambo ambalo wananchi wanapaswa kufahamu kupitia media.

“Kwenye Semina hii,waandishi wa habari mtafundishwa,muundo na majukumu ya Benki kuu,maana ya sera ya fedha inayotumia riba ya benki kuu,umuhimu wa benki kuu kuwa na dhahabu kama sehemu ya akiba yake ya fedha za kigeni,”amesema Gloria.
Ameongeza mafunzo mengine ni,utekelezaji wa sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha,uamuzi wa kundoa noti za zamani katika mzunguko,pamoja na kutambua Alama za fedha halali na utunzaji wake na kuzijua noti bandia.

Aidha,amesema kupitia mafunzo hayo, waandishi wa habari watafahamu pia sheria,kanuni na miongozo kuhusu taasisi ndogo za kifedha,ili kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi juu ya kuepukana na mikopo kausha damu au umiza na kujua haki na wajibu wao.
Meneja msaidizi Idara ya Mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania Dodoma Noves Moses,amesema mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, itasaidia wananchi kufahamu masuala ya benki kuu, na kuondoa maswali kupitia upashwaji wa habari.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza (MPC)Edwin Soko, akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari,amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao,ambapo watakuwa mabalozi wazuri wa benki kuu, katika kuandika maudhui bora ya habari na kuelimisha umma.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania Tawi la Mwanza Gloria Mwaikambo akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Meneja msaidizi Idara ya Mawasiliano kutoka Benki kuu ya Tanzania Dodoma Noves Moses akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi kutoka BoT Issa Pagali akitoa mafunzo.
Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Masoko ya fedha BoT Dkt.Anna Lyimo akitoa mafunzo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza (MPC)Edwin Soko akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo kutoka BoT.
Picha ya pamoja.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464