BoT yatoa mbinu wananchi kukwepa mikopo kausha damu
Na Marco Maduhu, MWANZA
BENKI kuu ya Tanzania(BoT)Tawi la Mwanza,imewataka wananchi kukopa fedha kwenye taasisi za huduma ndogo za kifedha ambazo zimepatiwa lesseni na benki hiyo.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 15,2025 na Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi kutoka BoT Issa Pagali,kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Kanda ya Ziwa.
Amesema ili wananchi waepukane na mikopo ambayo isiyo rafiki kwao, ni vyema wakakopa fedha kwenye taasisi za huduma ndogo za kifedha ambazo zimepatiwa lesseni na benki kuu, ambazo zina riba elekezi isiyozidi asilimia 3.5 kwa mwezi.
Mkurugenzi wa BoT Tawi la Mwanza Gloria Mwaikambo.
Amesema kupitia kwenye Website ya benki kuu,imethibitisha taasisi zote za kifedha ambazo zimepewa lesseni na benki hiyo,ambapo wananchi wanapaswa kuingia na kuona taasisi ndogo za watoa huduma za kifedha ambazo zina lessen kutoka BoT.
"Utoaji wa lesseni kwa watoa huduma ndogo za kifedha daraja la pili tumeshatoa lessen zaidi ya 2100 na maombi yapo mengi sana," amesema Pagali.
Aidha,amesema kwa mtoa huduma ndogo za kifedha ambaye ana lessen ya Benki kuu,akikiuka masharti ya lesseni hiyo na kutoza riba kubwa,adhabu yake ni kufutiwa lesseni.
Aidha,amesema mipango ya mbeleni kama benki kuu, ni kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari, kuhusiana na umuhimu wa kuelewa vigezo na masharti ya mikataba ya ukopeshaji na kupatiwa nakala ya mkataba uliosainiwa.
Pia kuwaelemisha wananchi juu ya athari za kukopa mikopo kwa watoa huduma ndogo za kifedha wasio na lessen kutoka benki kuu, pamoja na kujenga mfumo wa uwazi juu ya riba.
Amesema benki hiyo pia imeidhimisha utekelezaji wa kampeni dhidi ya mikopo umiza isemayo" zinduka,usiumizwe kopa kwa maendeleo" ambayo itatolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Naye Mkurugenzi wa BoT Tawi la Mwanza Gloria Mwaikambo,amewataka wananchi pia wanapoingia kwenye taasisi ndogo za watoa huduma za kifedha kwa ajili ya kukopa,wanapaswa waangalie lessen zao ambazo hubandikwa ukutani,pamoja na kusoma mikataba ya mikopo na riba yake, na kuchukua copy ya nyaraka aliyokopea fedha.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI 👇👇
PICHA NA KADAMA MALUNDE
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464