WANAWAKE KILOLELI WAHAMASIKA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

WANAWAKE KILOLELI WAHAMASIKA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Na Marco Maduhu,KISHAPU

KITUO cha Taarifa na Maarifa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)Kata ya Kiloleli wilayani Kishapu, wameeleza namna walivyohamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za ugongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kiloleli Kwangu Madaha.

Hayo yamebainishwa leo novemba 19.2024 na Mwenyekiti wa Kituo hicho Kwangu Madaha,wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amesema baada ya kujengewa uwezo na TGNP juu ya masuala ya wanawake na uongozi, kituo hicho kilitoa elimu kwa wanawake kupitia majukwaa mbalimbali na mikutano yao,kuhamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ili wapate fursa ya kushiriki kwenye vikao vya maamuzi na kupitisha ajenda zao.
“Muitikio wa wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu,umekuwa mkubwa sana,mfano nafasi zote za ujumbe, ambapo wanawake waliojitokeza kugombea wote wameshinda ndani ya Chama na wanasubili kupigiwa kura na wananchi novemba 27,”amesema Kwangu.

Aidha,amesema nafasi ya Uenyekiti alijitokeza yeye peke yake kugombea kuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiloleli, lakini kura zake hazikutosha ndani ya Chama (CCM)na kukomea kuwa mshindi wa Pili.
Ametaja baadhi ya sababu ambazo zilimfanya awe mshindi wa Pili kuwa ni tatizo la mfumo dume kwa kupigiwa kampeni chafu kuwa Kijiji hakiwezi kuongozwa na Mwanamke, pamoja na kutokuwa na fedha za kuwapatia wajumbe ili wampigie kura,na kuishia kuomba kura mikono tupu na kusababisha kushindwa.

Ameongeza kwamba licha ya tatizo mfumo dume bado lipo kwa jamii japo siyo wa ukubwa kama zamani, jamii pia imeanza kuwaelewa wanawake kushika nafasi za uongozi, na kwamba katika kuwania nafasi hiyo ya Uenyekiti wa kijiji Kiloleli, walikuwa wagombea 9, lakini yeye aliwabwaga wanaume wengine 7 na kushika nafasi ya pili.
Mwanamke mwingine Neema Shija, amesema yeye alishinda nafasi ya ujumbe wa Serikali za Mitaa katika Kijiji hicho cha Kiloleli ndani ya Chama (CCM), huku akihaidi wakishinda siku ya uchaguzi novemba 27 kwa kupigiwa kura na wananchi, atitumikia jamii vizuri pamoja na kusukuma ajenga za wanawake na watoto ndani ya vikao vya maamuzi.

Mwanaume Joseph Solea, amesema jamii bado inahijajika kupewa elimu zaidi juu ya kuachana na mfumo dume, na kuwapa nafasi za uongozi wanawake sababu ni watendaji kazi wazuri na waaminifu.
Aidha,Uchaguzi wa Serikali Mitaa utafanyika novemba 27 mwaka huu, kwa kuchagua viongozi nafasi ya Uenyekiti wa Kijiji, Vitongoji, Mitaa pamoja na wajumbe, ambapo uchaguzi wa ndani ya vyama umeshafanyika, na sasa wanaelekea kwenye kampeni ili wagombea wanadi sera zao kwa wananchi na kupigiwa kura.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464