RC MACHA AONGOZA MAHAFALI YA 43 CHUO CHA VETA SHINYANGA AWASIHI WAHITIMU KUTUMIA FURSA ZILIZOPO MTAANI


RC MACHA AONGOZA MAHAFALI YA 43 CHUO CHA VETA SHINYANGA AWASIHI WAHITIMU KUTUMIA FURSA ZILIZOPO MTAANI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ameongoza mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Mwaka wa Pili (Level Two) katika Chuo cha Ufundi Stadi Shinyanga (VETA), ambapo jumla ya wanachuo 198 wamehitimu mafunzo katika fani mbalimbali.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika leo, Ijumaa, Novemba 22, 2024, Mhe. Macha amewapongeza wanachuo kwa kumaliza mafunzo yao na kuwaonya kutumia elimu waliyoipata kwa malengo ya kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla.

“Serikali ipo kuhakikisha mnafikia ndoto zenu za maisha, kupitia mafunzo haya mliyoyapata, Mkachangamkie fursa zilizopo mtaani, ni wasihi nendeni mkachape kazi, mkawe waungwana na wavumilivu na mkatumie elimu yenu kwa usahihi ili kuboresha maisha enu na jamii kwa ujumla” amesema RC Macha.

Amesema serikali imejipanga kusaidia na kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa vijana, wanawake na makundi maalum ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi ya maendeleo hivyo amewataka wahitimu hao kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwenye kila halmashauri.

Aidha, Mhe. Macha ametilia mkazo umuhimu wa vyuo vya ufundi stadi, akisema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuboresha vyuo vya VETA nchini na kwamba serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya vyuo vya VETA, ikiwemo ujenzi wa uzio wa chuo hicho unaotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 400.

RC Macha pia ameipongeza VETA kwa kuanzisha mfumo wa kupika kwa gesi badala ya kutumia mkaa, akisema ni hatua nzuri katika kupunguza athari za mazingira.

Katika sehemu nyingine, Mhe. Macha amezungumzia umuhimu wa VETA kama kiungo muhimu katika ujenzi wa taifa, akisema vyuo vya ufundi stadi vinachangia pakubwa katika kutoa wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali, akiwemo umeme, ujenzi, na uchakataji wa madini.

Awali Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Mwl. Abraham Richard Mbughuni amesema idadi ya wanafunzi waliosajiliwa katika kozi za muda mrefu kwa sasa ni 525 na kozi fupi ni 753 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2024 hadi Novemba 2024.

Mwl. Mbughuni ameeleza changamoto zinazowakabili chuoni hapo ikiwemo ukosefu wa ukuta wa uzio unaozunguka chuo hicho ambapo takribani shilingi milioni 400 zinaitajika kukamilisha ujenzi huo huku akiitaja chngmoto nyingine kuwa ni uchakavu na uchache wa magari ya kujifunzia udereva wa awali, magari ya abiria, magari ya mizigo na mitambo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Mwl. Abraham Richard Mbughuni akisoma historia fupi ya chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Mwl. Abraham Richard Mbughuni akisoma historia fupi ya chuo hicho.
Mkurugenzi wa VETA kanda ya magharibi Asanterabi Kanza akizungumza wakati wa mahafali hayo ya 43 ya chuo cha VETA Shinyanga.
Mratibu wa mafunzoVETA Shinyanga Rashid Hamis Ntahigiye akizungumza wakati wa mahafali hayo ya 43 ya chuo cha VETA Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa VETA kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa VETA kwenye mahafali hayo.
Baadhi ya waalimu wa Chuo cha ufundi stadi VETA Shinyanga kwenye mahafali hayo ya mahafali ya 43 ya chuo cha ufundi stadi VETA Shinyanga.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza kwenye mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa Mwaka wa Pili (Level Two) katika Chuo cha Ufundi Stadi Shinyanga VETA.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha VETA Shinyanga walioudhuria mahafali hayo.
Baadhi ya wazazi na walezi walioudhuria mahafali hayo.
Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha alipotembelea mtambo wa uzalishaji umeme jua uliobuniwa na wanafunzi wa chuo cha VETA Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwasili kwenye viwanja vya mahafali hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwasili kwenye viwanja vya mahafali hayo.
Picha ya Pamoja.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464